Habari kuhusu Vita na Migogoro kutoka Februari, 2015
Watoto Waliokosa Masomo kwa Miezi kadhaa, Wafundishwa kwa Njia ya Skype Nchini Libya
Haifa El-Zahawi, raia wa Libya aishiye New York, kwa mara ya kwanza amewapatia fursa ya kusoma watoto wa nchi atokayo ya Libya kufuatia watoto hao kushindwa kwenda shuleni kwa miezi kadhaa sasa. Shukrani kwa mawasiliano kupitia Skype
Je, Kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu Naijeria Kunatokana na Sababu za Kiusalama?
Jeshi la Nigeria litaendesha operesheni maalum ya wiki sita dhidi ya Boko Haram ili"kuepusha kuingiliwa na shughuli za uchaguzi." Baadhi ya watu wanatilia shaka kuwa, kuahiririshwa kwa uchaguzi ni mkakati wa kisiasa.
Msichana Achora Ramani ya Palestina kwa Kutumia Risasi za Israeli Alizokusanya Karibu na Nyumbani Kwao
Picha hii ya msichana wa ki-Palestina inazunguka kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa zinasema msichana huyu alikusanya maganda ya risasi karibu na nyumbani kwao, akayatumia kuchorea ramani ya Palestina.
Vijana wa Naija Wacharuka Kufuatia Shambulizi la Boko Haram huko Bosso na Diffa
Kwa mara ya kwanza, Boko Haram kimetekeleza shambulio kwenye mpaka na Naija na vijana wa ki-Naija hakuweza kuvumilia. Boko Haram walishambulia Bosso na Diffa, miji miwili iliyo kusini mashariki mwa...
Boko Haram Yaua Watu Wasiopungua 81 Huko Fotokol, Cameroon Kaskazini
Mnamo Februari 4, Boko Haram walifanya shambulio baya kwenye mji wa Fotokol Kaskazini mwa Cameroon, baada tu ya kuvuka mpaka wa Naijeria. Mamia wa raia wanahofiwa kupoteza maisha 81 wamethibitika...
Raia wa Jordan Washitushwa na Video ya Mauaji ya ISIS, Wamkumbuka Mwanajeshi Aliyeuawa Kishujaa
Muonekano wa kutisha wa video ya mauji ya Rubani wa Jordan imewashitua wengi, lakini baadhi ya watu hawakukubali kuruhusu propaganda za ISIS za kuharibu kumbukumbu nzuri ya shujaa huyu aliyeuawa.
Wafilipino Wauliza ‘Rais Yuko Wapi?’ Baada ya Kutokuonekana Kwenye Mapokezi ya Polisi Waliouawa
Polisi arobaini na wanne walipoteza maisha yao kwenye operesheni maalum ya kumkamata mtu anayedaiwa kuwa mhusika mkuu wa mabomu ya Bali ya mwaka 2002. Rais Aquino alihudhuria uzinduzi wa kiwanda cha magari badala ya kupokea miili ya polisi hao