Habari kuhusu Vita na Migogoro kutoka Disemba, 2011
Korea Kusini: Dikteta Kim Jong Il wa Korea ya Kaskazini afariki dunia
Kim Jong Il, dikteta wa Korea Kaskazini amefariki. Japokuwa kifo cha dikteta huyo mwenye sifa mbaya duniani ni jambo ambalo watu wanapaswa kulipokea vyema, watu wengi wa Korea Kusini wameonyesha wasiwasi juu ya hali tete katika bahari ya Korea itakayotokana na kifo chake cha ghafla.
Mexico: Wanafunzi Wawili Wauawa Kwenye Maandamano Huko Ayotzinapa
Wanafunzi wawili, Jorge Alexis Herrera Pino na Gabriel Echeverría de Jesús, waliuawa tarehe 12 Desemba 2011, wakati wa maandamano ya wanafunzi wa shule ya vijijini ya Raúl Isidro huko Ayotzinapa, mji mkuu wa Guerrero, Chilpancingo, nchini Mexico. Mitazamo yenye utata kuhusu yalioyotokea imechapishwa mtandanoni.