· Disemba, 2012

Habari kuhusu Vita na Migogoro kutoka Disemba, 2012

Habari za Upotoshaji Kuhusu Afrika Katika Vyombo vya Habari vya Kimataifa

 Kampeni ya kumkamata #Kony2012 ilibeba mambo yaliyorahisishwa mno kuhusu Afrika. Vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe, hata hivyo, kwa sasa havina kinga dhidi ya ukosoaji wa aina hii. Hapa ni muhtasari wa watu maarufu, makosa na kutokuwepo umakini katika habari zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari vya dunia kuhusu Afrika na katika vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe

Assad atumia Ndege ya Kivita Kuwaua Raia Wake

Serikali ya Syria imefanya shambulizi kubwa la angani dhidi ya raia wa nchi hiyo -waliokuwa wamesimama kwenye foleni waisubiri mikate kwenye kiwanda cha kuokea miakte huko Halfaya, Hama. Inakadiriwa kwamba watu waliouawa katika shambulio hilo mjini humo ni kati ya 90 na 300, waasi wakisema kuwa watu hao walikuwa wamejitenga na vikosi vya Assad. Mtandaoni, wanaharakati wanashangazwa inakuwaje dunia inaendelea kutazama tu maisha ya watu wasio na hatia wakiuawa kwa mamia.