Habari kuhusu Vita na Migogoro kutoka Novemba, 2008
Iraki:OBAMAAAAA!!! Huraaah Oyee!!
Hivyo ndivyo asemavyo Neurotic Iraqi Wife. Kwa ujumla blogu nyingi za Iraki zimemchukulia vyema rais mteule Obama, lakini sio wanablogu wote waliofurahia. Salam Adil anaorodhesha maoni baada ya Uchaguzi wa rais huko Marekani.
Kongo: Utata Watawala Goma
Miezi miwili iliyopita mapigano yamezuka tena katika jimbo la mashariki la Kivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya kundi la upinzani linaloongozwa na Jenerali laurtent Nkunda na majeshi ya serikali, kinyume na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi januari. Mapambano hayo yameongezeka zaidi katika siku 6 zilizopita na, japokuwa usitishaji wa vita hivyo ulitangazwa, hali bado ni ya kutananisha mjini Goma. Yafuatayo ni maoni kutoka kwa wanablogu walioko sehemu hiyo.