Habari kuhusu Vita na Migogoro kutoka Novemba, 2009
Brazil: Mtazamo wa Wakazi wa Vitongoji Maskini
Katika makala hii, tunasikia mitazamo ya wanahabari raia kutoka mradi wa Viva Favela kuhusiana ya vurugu inayotokana na mihadarati huko Rio de Janeiro na jinsi inavyofagia makazi ya walalahoi, kama wanavyoiona mbele ya milango ya nyumba zao.
Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini
Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.
Kenya: Mwai Kibaki na Odinga Budi Washirikiane na ICC
Ubia wa Kuleta Mabadiliko umetoa tamko linalowataka mwai kibaki na raila odinga kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya Jinai na kuhakikisha muswada wa Tume Maalum unapitishwa nchini kenya na kurasimishwa...
Vijana wa Kiyahudi na Kipalestina Watumia Video Kuuelewa Mgogoro
Mashirika mawili tofauti nchini Israel na katika Majimbo ya Palestina yanatumia zana za video ili kuwasaidia vijana wa Kiarabu na Kiyahudi kuuelewa mgogoro na kujenga daraja kati yao.