Habari kuhusu Vita na Migogoro kutoka Aprili, 2011
Côte d'Ivoire: Kuanguka kwa Laurent Gbagbo
Laurent Gbagbo alikamatwa katika makazi yake ya Cocody, pamoja na mkewe, Simone, na msafara wa watu wa karibu. Miezi mitano baada ya kukataa kukabidhi madaraka kwa rais anayetambuliwa kimataifa kama rais mpya wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, mgogoro nchini humo hivi sasa unaelekea kufikia hitimisho.Mtiririko wa matukio yaliyopelekea kukamatwa kwa Gbagbo yaliorodheshwa kwa kina kwa njia ya video za kwenye mtandao ambazo zilitolewa maoni kwenye mtandao.
Côte d'Ivoire: Gbagbo agoma, Waafrika waandamana
Wakati Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Rais Laurent Gbagbo akiwa bado amejichimbia ndani ya handaki nchini humo, akigoma kukamatwa kwa kuendelea kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, ushiriki wa Ufaransa katika harakati za kumng’oa zinasababisha miitikio miongoni mwa wanasiasa na raia wa Ufaransa, pamoja na jamii ya Waafrika waishio Ufaransa.
Côte d'Ivoire: Abijani kwenye masaa ya kudhoofu kwa utawala wa Gbagbo
Siku mbili zilizopita zimekuwa na utajiri katika misuguano na mivutano nchini Côte d'Ivoire. Vikosi vinavyomtii Ouattara, vilianza mashambulizi kuelekea Kusini na Magharibi mwa nchi hiyo. Katika siku zisizozidi tatu, walifanikiwa kuikamata miji ya Douékoué na kufika Yamoussoukro tarehe 30 Machi. Wa-Ivory wanatoa maoni yao kuhusu wafungwa kutoroka, kufungwa kwa televisheni ya taifa na sehemu aliyo Gbagbo:
Côte d'Ivoire: Televisheni ya Taifa RTI Inawezekana kuwa Inatangaza Kutokea Kwenye Gari la Matangazo
Kama vile alivyoelezea Julie Owono , ni vigumu kupembua mapambano ya kudhibiti vyombo vya habari vya Pwani ya Pembe (Cote d'Ivoire). Taarifa kutoka Waandishi Wasio na Mipaka inaashiria kuwa RTI...