Iraki:OBAMAAAAA!!! Huraaah Oyee!!

Hivyo ndivyo asemavyo Neurotic Iraqi Wife. Kwa ujumla blogu nyingi za Iraki zimemchukulia vyema rais mteule Obama, lakini sio wanablogu wote waliofurahia.

Layla Anwar anabashiri jambo baya kwa Iraki wakati wa uraisi wa Obama:

Kwa hiyo Obama, booma[Booma ni bundi lakini katika lugha mojawapo ya Kiiraki neno hilo linamaanisha mtu mjinga ]…

Makamu wa raisi wa booma si mwingine zaidi ya J.Biden. J.Biden, Mzayonisti, muungaji mkono ngangari wa kuigawa Iraki katika majimbo matatu. Si ajabu Maliki na washirika wake wanamuunga mkono booma ubavuni na Irani….Nina furaha kwamba muovu, mwanaharamu Bush anaondoka. Sina shaka kwa hili. Lakini sitawapongeza kwa raisi wenu wa 44. Atakacho fanya ni kumalizia yale mazayonisti wenzake waliyoyaanza- Kuigawanya nchi yangu.

Ishieni jahanamu nyote pamoja na maraisi wenu

Kusema kwamba Neurotic Wife anafurahishwa na uchaguzi wa Marekani ni sawa kupunguza makali ya matamshi yake. Anaandika:

Mabadiliko, mabadiliko, mabadiliko. Mabadiliko yako njiani. Mabadiliko kwa utawala wa kidhalimu wa Bush. Utawala wa Bush uliodanganya,uliolaghai, uliodhulumu dunia, na zaidi ya yote uliowadhulumu Wairaki… Kwangu mimi, hili si jambo linalohusu historia tu, hii inahusu mtu aliyeweza kuwashusha watu walioivunja nchi yangu. Ni konde kubwa kwa kila mtu alieangamiza Wairaki. Na kwangu mimi ni ushindi wa kutosha.

Nitapenda tu kumwambia Bwana Obama, usituangushe. Umetoka mbali, na kama Muiraki ninakutegemea. Usiziruhusu siasa chafu kukuvunjia ahadi zako… Nimejifunza mambo kadhaa katika maisha yangu, nayo ni katu kamwe usitegemee sana mambo kutoka kwa watu, lakini kwa hili nina matumaini. Nategemea mambo mengi toka kwa Obama. Na la kuangushwa SI mojawapo. Kwa wale wafuasi wenye siasa kali wa mlengo wa kulia, na kwenu nyote ambao hamtaki kukubali kuelewa Mmarekani mweusi anaweza kuwa raisi wenu, bahati mbaya. Ishi nalo…

Ni anga ya kupendeza leo. Anga ya KIBULUU. Mwanzo wa zama mpya. Zama za Obama…

Na Fatima Mmarekani mwenye asili ya Iraki hatimaye anajivunia. Anatanabaisha:

Kwangu mimi, najivunia Marekani sasa hivi. Najivunia kwa kuyashinda mengi, kwa kutuonyesha yale ambayo inweza kuyafanya.
Na kwangu mimi, nina matumaini kuwa Obama hatatuangusha. Nina matumaini ataliongoza taifa hili kufikia misingi ya sheria na usawa kwa wote, na kwamba atakaa mbali na vitendo vya kibabe, popote itakapokuwa. Natumaini hatakuwa mmoja wa wale maraisi.
Na mwisho nampongeza John McCain kwa kazi yake na hotuba yake usiku wa jana. Ilikuwa ya kuiungwana, ninatumaini atapumzika baada ya miaka mingi ya utumishi.

GOOOBAMA! Idumu Haki, Usawa na haya yote mazuri katika katika hii dunia

Na mwisho

Namalizia na ujumbe huu wa pongezi kutoka kwa Wairaki kwenda kwa wamarekani

Iraqi Mojo:

Wamarekani wamechagua Muamerika mwenye asili ya Kiafrika aitwaye Barack Hussein Obama kuwa raisi wao. Mungu ibariki Marekani!

Sahar:

Nina furaha kwa Iraki? Sijui. Sijui nini kitatokea na ninaogopa.

Je ataondoa majeshi?
Je atajali vilivyo na kufikia makubaliano mazuri – yaliyo sawa kwa watu wa Iraki?

Lakini pamoja na mashaka yangu yote, naionea raha Marekani – Mmetoka mbali. Mmlikuwa na ujasiri, na nia ya kumchagua mtu wa mabadiliko. Na kwa moyo wangu wote natumaini ataiweka marekani katika njia ya kupona.

Kuiona Marekani upya katika misingi ya uhuru na demokrasia, nguvu pole ambayo inapoza badala ya kuumiza, inaunganisha badala ya kugawanya – punde inshalla.
Napenda kuwapongeza nyote.

Iraq Pundit:

Kwa miaka kadhaa mara kwa mara nimejikuta nawatetea Wamarekani wanapokosolewa na wapinzani wao kama vile Wafaransa na Waarabu,ambao wanadai kuwa watu wa Marekani ni mazuzu wabaguzi hayawani. Nimejaribu kuongea na wakosoaji hao, lakini sikufika popote. Pengine kuchaguliwa kwa Baraka Obama kama raisi wa Marekani kutawafumbua jinsi gani walikosea… Ni wale tu wasio na mioyo ambao hawakusisimuka jana usiku wakati Obama alipotangazwa mshindi wa kiti cha urais… Kwa hiyo hongera kwa Barack Obama. Asitokee mtu na kusema hii sio nchi ya kustaajabisha.

Na kutoka Baghdad, Marshmallow26:

Hongereni wapendwa Wamarekani katika uchaguzi na kwa raisi mpya. Haijalishi matokeo yalivyokuja mna matumaini nasi tunatumaini raisi mpya ataleta mustakabali wenye mwangaza kwa Marekani na kwa Iraki.
Zaidi ya Wamarekani milioni 130 wamepiga kura. Hii ni idadi kubwa.
Kitu nilichokipenda kwa wamarekani ni kuwa hawakulipa kipaumbele suala la rangi katika kupiga kura, wengi wa watu weupe walimpigia kura Obama ambae ana nasaba ya Kiafrika, kwa sababu hawaamini katika rangi au dini lakini kanuni za nchi na watu wake…

kwa mara nyingine tena Mabrook :)

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.