Korea Kusini: Dikteta Kim Jong Il wa Korea ya Kaskazini afariki dunia

Kim Jong Il, dikteta aliyetawala ufalme wa Korea Kaskazini kwa miongo mitatu, amefariki akiwa na umri wa miaka 69. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa Jumatatu , kupitia runinga ya taifa, Kim alifariki kwa sababu ya “uchovu wa kiakili na kimwili” wakati akisafiri kwa gari moshi mnamo tarehe 17 Desemba, 2011. Watumiaji wa twita wa Korea Kusini walilipuka wakionyesha hisia mchanganyiko. Ingawa kifo cha dikteta huyo katili zaidi duniani ni tukio ambalo raia wengi wa Korea Kusini wangelifurahia, wengi wameonyesha mashaka kwa kuwa tukio hilo lilimaanisha kuanza kwa hali tete ya usalama inayoweza kusababishwa na kifo hicho katika pembe ya bahari (peninsula) ya Korea.

Mwitikio wa awali kabisa wa wananchi wa Korea Kusini kwa habari hizi ulikuwa ni taharuki. Son Byung-gwan(@sonkiza), mwandishi wa wavuti wa habari za kiraia za Korea Kusini Ohmynews,  alituma ujumbe huu kwenye twita: [ko]:

북한, 김정일 사망 속보… 너무 큰 뉴스라서 편집국도 어리둥절

Korea Kaskazini imeripoti habari ya hivi punde ya kifo cha Kim Jong-il. Habari hii ni kubwa kiasi kwamba hata dawati la habari katika kampuni yetu lilistushwa

Picha ya Kim Jong-il
Kim Gil-su (@yourKGSalituma ujumbe kwenye twita [ko]:

김정일 사망 소식에 속이 후련한 것보다 걱정이 앞네요. 나이가 들어서인가봐요.

Badala ya kujisikia ahueni, ninajihisi hofu kufuatia habari za kifo cha Kim Jong-il. Labda ni kwa sababu mimi ni mzee.

Wengi kwenye Twita walihofia pia kwamba madai ya kuwapo vitendo vya udanganyifu katika uchaguzi vilivyokihusisha chama kinachotawala yangefunikwa na habari hizi @photo_jjang aliandika [ko]:

모든 언론사 홈페이지에 올라온 김정일 사망소식 뉴스…. 그 밑에 이슈들은 다 묻히는겁니다

Katika kurasa za mbele za vyombo vyote vya habari, kifo cha Kim Jong –il kimegonga vichwa vya habari…hiyo ikimaanisha masuala mengine yote (yanayochapishwa na yasiyohusiana na habari hiyo) hayatapata wasomaji.

Baada ya mawimbi ya awali ya mshtuko, wachangiaji wengi kwenye Twita walianza kuilaumu serikali ya Korea Kusini kwa mwitikio wake hafifu. Inaaminika kwamba hawakuwa na taarifa juu ya kifo cha Kim kwa zaidi ya saa 50. Kwa sasa, Rais wa Korea Kusini Lee ametangaza hali ya hatari.  Barry Lee (@barry_leealiandika [ko]:

김정일이 죽은게 17일인데 이명박은 17, 18일에 방일을 했군요.정말 몰랐다면 정보력이 개판이라는 소리고 알고도 다녀왔다면 위기 대응 능력이 개판이라는 소리군요. […]

Kim alifariki Desemba 17. Na Rais Lee Myung-bak alikuwa ziarani nchini Japan tangu Desemba 17 hadi 18. Kama ni kweli Rais Lee hakuwa amesikia habari hizi, maana yake idara ya usalama wa taifa ya Korea Kusini inatia aibu. Au kama alijua, hiyo ina maana kwamba yeye ni dhaifu sana katika kukabiliana na hatari.

Twita za Korea Kusini wakati huo zilijaa tafakari juu ya mustakabali wa taifa lao na athari za tukio hilo kwenye amani ya pembe ya bahari ya Korea. Mtumia Twita CaféVine (@CafeVine) alituma ujumbe huu[ko]:

가장 큰 불안요소는 북한 군부의 소요 가능성이 아니라 주변 강대국의 정치 계산에 의한 움직임과 북한 민중의 반응이 아닐까 싶다. 북한 군부가 흐트러지는 틈을 타 대규모 탈북 움직임이 일어난다면… 위험하다.

Maeneo hasa yanayosababisha hali tete SIO uwezekano wa uasi ndani ya jeshi la Korea Kaskazini, LAKINI mabadiliko ya hali ya kisiasa katika pembe ya Korea kwa kusababishwa na hatua zitakazochukuliwa na mataifa yenye nguvu na vilevile hatua zitakazoweza kuchukuliwa na raia wa Korea Kaskazini. Itakuwaje kama kutakuwa na ongezeko la ghafla la raia wa Korea Kaskazini wanaoikimbia nchi hiyo kwa sababu ya hali tete kwenye jeshi la nchi yao? Hiyo inaweza kuwa hatari.

@trimutri100 alionyesha hofu yake kwa kwa mrithi wa Korea Kaskazini, asiye na uzoefu, kijana mdogo wa miaka 27 tu, Kim Jong-un:

북한은 진정 큰일이구나. 그 햇병아리가 정권을 제대로 인수할리도 없고, 차라리 김정남이 긴급 호출되는게 아닐까?

Korea Kaskazini ni janga kamili. Huyu kinda (akimaanisha Kim Jong-un) hataweza kabisa kupokea madaraka ya utawala …Je, kuna uwezekano wa wao kutuma wito wa dharura kumsaidia Kim Jung-nam [mwana mkubwa wa Kim Jong-il]?

Baadae alitoa maoni [ko]kwamba kutokana na ukweli kuwa habari hizo zilitolewa na chombo cha habari cha serikali ya Korea Kaskazini, maana yake hali imedhibitiwa:

북한이 발표를 했다는 건, 권력구도가 최소한 어느 정도는 교통정리가 되었다는 이야기다. 문제는, 그게 누구냐는거다.

Kutokana na ukweli kwamba Korea Kaskazini ndiyo iliyotangaza habari hizo, hiyo ina maana kwamba kupokezana madaraka kumechukua sura nzuri. Lakini tatizo linalobaki hapa ni NANI amechukua madaraka…

Fuatilia Global Voices ili kupata habari zinazoendelea kutufikia kupitia @globalvoices.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.