Wafilipino Wauliza ‘Rais Yuko Wapi?’ Baada ya Kutokuonekana Kwenye Mapokezi ya Polisi Waliouawa

"RETWEET if you think PNoy should've attended the arrival of honors instead of that Car Plant event. #NasaanAngPangulo" tweets @BobOngWords.

“TWITI TENA kama unadhani PNoy alipaswa kuhudhuria mapokezi ya heshima badala ya tukio la Kiwanda cha Magari. #NasaanAngPangulo” alitwiti @BobOngWords.

Alama habari #NasaanAngPangulo, yenye maaana ‘Rais yuko wapi’ katika lugha ya Kitagalog, ilikuwa mada maarufu zaidi kwenye mtandao wa Twita duniani wakati Wafilipino walipokuwa wakionesha hasira zao kwa Rais Noynoy Aquino kufuatia  kukosekana kwake kwenye mapokezi ya heshima ya miili ya polisi waliouawa wakiwa kwenye operesheni maalum.

Aquino alihudhuria kuzinduliwa kwa kiwanda kipya cha magari cha kampuni ya Mitsubishi huko Laguna (jimbo lililo kusini mwa Manila) badala ya kuhudhuria mapokezi ya miili ya polisi. Majeneza yaliyobeba mabaki ya miili ya polisi hao yaliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Villamor baada ya kusafirishwa kutoka Mamasapano, mji ulio kusini mwa Ufilipino, Maguindanao.

Askari arobaini na wanne wa Jeshi la Polisi la Ufilipino – Kikosi Maalum (PNP-SAF) waliuawa kwenye operesheni ya kupambana na ugaidi mapambano yaliyochukua masaa 11 kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Moro wanaotaka kujitenga na wanaofanya shughuli zao kwenye eneo la Mamasapano.

Marehemu hao walikuwa sehemu ya askari 400 waliokuwa wametumwa kumkamata mtu anayedaiwa kupanga matukio ya milipuko ya mabomu ya Bali mwaka 2002 anayesemekana kujificha eneo hilo. Serikali ya Marekani ilitoa kiasi cha dola za Marekani milioni tano kama zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazowezesha kumkamata mtuhumiwa Zulkifli bin Hir alias Marwan.

Mfululizo wa ujumbe uliokuwa ukienea kwa kasi kudhihaki kukosekana kwa Rais Aquino kwenye mapokezi hayo ulizunguka kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Twita.

Wafilipino watumiao mitandao walikumbushana namna Rais Aquino alivyokuwa mwepesi kutoa muda wake kuhudhuria shughuli za zinazoandaliwa na makampuni makubwa wakati akikosekana kwenye majanga mengi makubwa yaliyoliathiri taifa.

Shughuli anazohudhuria Rais wetu!

Wengine walikumbushia jinsi rais alivyowahi kusema, “Sihudhurii shughuli za watu nisiowajua” alipoulizwa kwa nini hakuhudhuria maziko ya Jennifer Laude, aliyedaiwa kuuawa na mfanyakazi wa Marekani mwaka uliopita.

Mwandishi Katrina Stuart-Santiago alijaribu kufananisha umuhimu unaooneshwa na wakuu wengine wa nchi kwenye kutoa heshima zao kwa watu wanaoolifia taifa na kutokuonekana kwa rais Aquino kwenye mapokezi ya mashujaa hao kwenye bandiko lake la Facebook:

Wakati miili ya waathirika wa ndege ya MH17 ilipowasili nchini Uholanzi, Mfalme wa nchi hiyo Willem-Alexander na Malkia Maxima, na pamoja na familia karibu yote ya kifalme, wakiambatana na maafisa wa serikali walikaa na kutazama na kulia na kuomboleza na taifa wakati majeneza yaliposhushwa kutoka kwenye ndege. Hakuna kilichokuwa muhimu zaidi ya kuwaenzi marehemu hao.

Rais Aquino alitoa hotuba wakati ibada ya mazishi ya polisi waliouawa  siku moja baada ya majeneza kuwasili. Lakini wakati huo kwa mara nyingine alisemekana kuchelewa na kufanya shughuli zingoje mpaka atakapowasili.

Hotuba ya Aquino wakati wa ibada hiyo iligeuka kuwa kituko mtandaoni kwa kusemekana kuzungumzia mambo yake binafsi kuliko marehemu. Utani uliokuwa ukisambaa mtandaoni ulionesha namna Aquino huanza hotuba yake kwa maneno ya George Lucas wa Star Wars.

From the Facebook page of Jason Valenzuela.

Kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Jason Valenzuela.

Msemaji wa rais ametetea kutokuwepo kwa rais katika mapokezi ya miili ya polisi, akisema kwamba hiyo haikuwa sehemu ya ratiba yake. Pia alikejeli wakosoaji wake mtandao kwenye taarifa yake Ikulu, akisema kwamba ukosoaji huo ni mtazamo usiowakilisha maoni ya wengi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.