Raia wa Jordan Washitushwa na Video ya Mauaji ya ISIS, Wamkumbuka Mwanajeshi Aliyeuawa Kishujaa

1507741_10153086998904859_9192611209393606557_n

Kutoka kwenye video iliyotayarishwa na mtandao maarufu wa Kharabeesh kwa ajili ya kumbukumbu ya rubani aliyefariki, iliyowekwa katika ukurasa wa Facebook.

Mamia ya watu wa Jordan waliandamana  huku wakitoa matamko ya kuonesha kuliunga mkono taifa la Jordan masaa kadhaa mara baada ya kuonekana kwa video isiyoaminika mnamo Februari 3 iliyoonesha mauaji ya kutisha ya rubani wa Jordan aliyefahamika kwa jina la Luteni Muath Al-Kaseasbeh.

Video hii iliyopakiwa na  alghadnewspaper  katika mtandao wa YouTube inaonesha watu wakipaza sauti zao kwa kusema “tutazitoa sadaka roho zetu na damu yetu kwa ajili yako, Jordan’ na pia, walibeba mabango yaliyosomeka, “Kifo cha ISIS (Kifupisho cha neno la kiarabu ISIS).”

Baadhi ya waandamanaji walishinikiza kunyongwa kwa Sajda Rishawi, ambaye alikamatwa mara baada ya kushindwa kujitoa mhanga pale bomu alilokuwa amelivaa kushishindwa kulipuka. Hapo awali, ISIS walitaka Rishawi aachiwe kama sehemu ya makubaliano na serikali ya Jordan na ISIS ya kumwachia Luteni Muath Al-Kaseasbeh, ambaye  alikamatwa na askari wa ISIS mara baada ya ndege yake kutunguliwa mnamo tarehe 3 Desemba, 2014 nchini Syria.

Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislam ya Jordan   iliitisha   sala ya maombolezo itakayofanyika katika misikiti ya Mfalme tarehe 4 Februari na pia kuyataka makanisa yote ya Jordan yaomboleze kifo cha shujaa huyu kwa kuzipiga kengele za makanisa kwa taratibu na kwa mfululizo.

Katika kuonesha kushikamana na rubani huyu, kumekuwa na mpasuko katika ulipizaji kisasi

Kurasa za twita  zinazoelekeza kwenye picha zilizopigwa kutoka kwenye   video inayodhaniwa kuwa ni ya mauaji na zinazoonekana kuambatana na maeneo ya kijiografia ya jiji la Ar-Raqqah linaloshikiliwa kwa ukaribu kabisa na ISIS. Jiji hili lililoharibiwa vibaya kwa vita lipo katika jimbo la Aleppo nchini Syria. Televisheni ya taifa ya Jordan ilitaarifu kuwa, Al-Kaseasbeh inadhaniwa kuwa aliuawa tarehe 3 Januari, lakini kwa namna video hii inavyoonekana, imewashitua wengi ambao hawakutaka propaganda za ISIS kurejesha kumbukumbu yake. 

An Amman-based mtumiaji wa Twita afafanua:

mwandishi wa habari wa Syria na mchambuzi, Hassan Hassan afafanua kuwa wakati baadhi ya raia wa Jordan wanategemea kuwa serikali yao itatoa adhabu kali kufuatia kifo cha rubani wao, hatua hii inawezekana kuwa haina uhalisia:

ambaye ni mwanablogu wa Jordan na mmoja wa waanzilishi wa 7iber, Naseem Tarawnah ataka kuwepo kwa mjadala wa kitaifa, kwa hofu ya kutokujua mustakabali wa Jordan siku za usoni ikiwa mambo kama haya hayatachukuliwa kwa uzito wake:

Mwanaharakati aliyeko uhamishoni, Iyad El-Baghdadi asema kuwa ili kuwepo kwa mabadiliko, hakuna budi kwanza kukata mzizi wa fitna miongoni mwetu:

Usiisambaze video hii

Video ya mauaji ya dakika 22 inayoonesha Al-Kaseasbeh akichomwa moto hadi kufa akiwa amefungiwa kwenye kibanda, ikiwa imeboreshwa na kuhaririwa kwa kiasi kikubwa. Video hii inajumuisha nembo ya ISIS, sehemu ya mahojiano na rubani huyo, habari za kukamatwa kwa rubani huyu pamoja na picha za vita. 

Randa Habib wa AFP alitaarifu kuhusu namna ndugu wa karibu wa rubani huyu walivyoipokea taarifa hii:

Video hii ya kutisha, ikiwa katika mfumo wa video ya kuhaririwa, ilisambaa kwa haraka sana katika mitandao ya kijamii. Watu wengi walihamasisha kutokusambaza video hiyo kama moja ya juhudi za kuheshimu ndugu wa familia pamoja na kutunza heshima yake.

Jude Qattan, a mwanafunzi wa chuo kikuu na raia wa Jordan alitaka video hii kutokusambazwa mitandaoni:

Pia, mwandishi wa habari Andy Carvin alieleza jambo la maana dhidi ya usambazaji wa video hii:

Bridget Johnson aishiye Washington DC alipendekeza Al-Kaseasbeh akumbukwe kama rubani wa kutukuzwa wa Jordan:

Akiweka picha ya Al-Kaseasbeh akiwa Istanbul, mwandishi wa BBC, Faisal Irshaid alisema kuwa “hii ndio njia mbadala ya namna tunavyoweza kumkumbuka”:

Kwa upande mwingine, wale walioiona video hii, walishtushwa na walichokiona na kufananisha kitendo cha kumchoma mtu kwa moto hadi kufa kuwa ni ukatili usiovumilika. Tarawneh alisema kuwa dakika hizo 22 zilikuwa mbaya kabisa kuwahi kushuhudia katika maisha yake:

mwanablogu wa Misri, akitwiti kwa jina la The Big Pharaoh, alilifananisha kundi la ISIS na Nazis:

Muath, shujaa

Pia kupitia kiungo habari #IamMuath na #كلنا_معاذ katika lugha ya Kiarabuin Arabic, watu wengi walionesha mhikamano wao na familia ya Muath katika kumkumbuka kwa uzalendo wake wa kuitumikia nchi yake. Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jordan kwenye Umoja wa Mataifa Dina Kawar alimchora Al-Kaseasbeh kama shujaa mwerevu na ambaye ni alama ya ushujaa:

Buzzfeed's Sheera Frenkel pia alizungumzia familia yake kwa juhudi zao ambazo hazikukoma za kujaribu kuhamasisha kuachiwa huru kwa ndugu yao:

Moja ya mambo yaliyojadiliwa hivi karibuni ilikuwa ni kuendelea kupotea kwa thamani ya utu wa binadamu. Mpiga picha wa Jordan, Amer Sweidan alikusanya maoni ya wengi katika twiti yake:

Mohamed Abdelfattah ambaye ni mwandishi wa habari aliye na makazi yake huko Misri, alijikuta asiyekuwa na la kusema pale alipokuwa akifuatilia habari:

Siku moja kabla, watu wa Jordan walionesha mshikamano wao na Japan kufuatia ISIS  kushukiwa kutoa video iliyokuwa inaonesha kuchinjwa hadi kufa kwa mwandishi wa habari Kenji Goto.  Iliaminiwa kuwa, Muath Al-Kaseabeh, alikuwa mmoja wa mateka waliokuwa pamoja na Goto.

Kharabeesh, mtandao wa habari wa Jordan, uliweka katika mtando wa Facebook video ya kumbukumbu ya kifo cha rubani huyu. Katika kipindi cha masaa 3, video hii ilikuwa tayari imeshatazamwa mara 130,000. 

Deena Abu Mariam alitwiti mabango yaliyoandaliwa Jordan yaliyoonesha kupinga ugaidi, na pia yaliyoonesha kuiunga mkono nchi ya Japan:

Malkia wa Jordan, Rania Al Abdullah alitoa heshima ya pekee kwa Al-Kaseasbeh kwa kutambua mchango wake wa kulitumikia taifa la Jordan kwa ushujaa:

Uliapa kiapo na ulitimiza ahadi yako. Wewe umekubali kuifia nchi yako. Mungu aipumzishe roho yako.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.