Je, Kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu Naijeria Kunatokana na Sababu za Kiusalama?

The main opposition candidate Jenerali (Mstaafu) Muhammadu Buhari akiongea kwenye Kongamano la Raia wa Afrika wanaoishi Ughaibuni lililofanyika katika jiji la London. Baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa kuahirishwa kwa uchaguzi ni mbinu za kisiasa zilizo na lengo la kukipendelea chama tawala. Picha na Michael Tubi

Mgombea Urais wa upinzani, Jenerali (Mstaafu)
Muhammadu Buhari akiongea kwenye Kongamano la Raia wa Afrika wanaoishi Ughaibuni lililofanyika katika jiji la London. Baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa kuahirishwa kwa uchaguzi ni mbinu za kisiasa zilizo na lengo la kukipendelea chama tawala. Picha na Michael Tubi, copyright © Demotix (5 April, 2013)

Tume huru ya uchaguzi ya Nigeria (INEC) mnamo tarehe 7 Januari, 2015 ilitangaza kuwa, uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 14 Februari ungesogezwa mbele kwa muda wa wiki sita kwa sababu ya masuala ya kiusalama hususani katika maeneo yanayoshikiliwa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.

Kundi la Boko Haram linaendeleza harakati zake za machafuko Kaskazini mwa Nigeria. Siku za hivi karibuni, kundi la Boko Haram lilitekeleza kile kinachoelezewa na shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, kuwa ni “moja ya mauaji ya halaiki ambayo hayakuwahi kufanywa na kundi hili” katika mji wa Baga ulio Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Borno.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Attahiru Jega alisema kuwa jeshi litaendesha operesheni ya wiki sita dhidi ya Boko Haram ili “kuepusha kuingiliwa na masuala ya uchaguzi” Serikaliimejinadi kulifutilia mbali kundi hili ndani ya wiki sita.

Katika historia ya Naijeria, hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi mkuu wa Rais kuahirishwa. Hata hivyo, hii haitakuwa mara ya kwanza kwa uchaguzi wa Kitaifa kuahirishwa nchini Nigeria. Mwaka 2011, tulitaarifu kuhusu malalamiko ya watumiaji wa Mtandao wa intaneti wa Nigeria kuhusiana na mabadiliko ya tarehe za chaguzi za Taifa za kibunge.

Tangu kutangazwa kuahirishwa kwa uchaguzi, kumekuwa na ufuatiliaji wa karibu wa kutaka kujua hasa sababu za msingi zilizopekea kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa Rais. Kwa mfano, ‘Gbénga Sèsan, mkurugenzi wa Paradigm Initiative Nigeria, anafikiri kuwa tume ya uchaguzi ilishinikizwa kuahirisha uchaguzi:

Ni dhahiri kuwa uamuzi huu wa kuahirisha uchaguzi na @inecnigeria, ulilazimishwa. Hili lina matazamio makubwa ikizingatiwa

Henrik Angerbrandt, ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya uzamivu (PhD) katika masuala ya Sayansi ya Siasa na mtafiti katika taasisi ya Nordic Africa, anaamini kuwa kuahirishwa huku kwa uchaguzi kumechagizwa na sababu za kisiasa zaidi kuliko za kiusalama. Anashangaa ni kwa nini operesheni dhidi ya magaidi hawa waliokuwepo kwa miaka sita sasa inafanyika katika kipindi cha tarehe za uchaguzi wa Rais.

Aandika:

Takribani wiki tatu zilizopita, mshauri wa Rais wa masuala ya usalama wa taifa alipendekeza kuahirishwa kwa uchaguzi. Hata hivyo, uamuzi huu haukutokana na sababu kuwa, vyombo vya usalama havikuwa vimejiandaa, lakini ni kwa sababu ya usambazaji wa polepole wa kadi za wapiga kura. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), ambayo ndiyo mamlaka husika, ilitoa taarifa yake kuwa hakukuwa na sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi. Hivyo, inaonekana kuwa, kilichosalia ilikuwa ni kurejea kwenye kigezo cha masuala ya usalama ambacho, hapo awali, mwezi Septemba kilitolewa ufafanuzi na mwenyekiti wa Seneti ya Chama cha PDP.

Kuna nadharia tofauti za namna ambavyo chama tawala cha PDP kinavyofaidika na kuahirishwa kwa uchaguzi wa Rais. Kadiri siku za kupiga kura zilivyokaribia, kura za maoni zimeonesha ongezeko la wananchi waliokosa imani na sserikali ya Rais Goodluck Jonathan na hivyo Mwanajeshi mstaafu Muhamudu Buhari ameonekana kuwa anaweza kushinda kwenye uchaguzi huo. Kuahirishwa kwa uchaguzi kunaweza kutoa mwanya kwa Jonathan kurekebisha baadhi ya makosa aliyokwisha kuyafanya. Kama chama kilicho madarakani, PDP kinadhaniwa kuwa ni chama kinachoweza kusaidiwa zaidi na serikali kuliko [All Progressive Congress] APC, hali inayochangia kupelekwa mbele kwa muda wa uchaguzi kwa manufaa ya chama tawala. Pamoja na kuwa Rais Goodluck Jonathan hakutaka nchi jirani kuisadia nchi yake kupambana na Boko Haram, ushirika wao katika wiki chache unaweza kuisaidia Naijeria kusitisha harakati za magaidi hawa za kutaka kuitawala nchi hii, jambo ambalo linaweza kuchukuliwa kuwa ni moja ya manufaa itakayopata chama tawala kutokana na kuahirishwa jwa uchaguzi. Hali ambayo Kuahirishwa kwa uchaguzi kunaweza kutoa mwanya kwa Uwezekano mwingine wa chama tawala kufaidika na kuahirishwa kwa uchaguzi. Hili litamfanya Jonathan arudishe imani kwa wale wapinzani wake wanaohoji uwezo wake na utayari wake wa kukabiliana na Boko Haram.

Anatanabaisha kuwa kuahirishwa kwa uchaguzi kumegubikwa na hali ya watu kuonesha kukatishwa tamaa pamoja na ni uamuzi wa mashaka tele. Anajiuliza ni nini kitatokea ikiwa malengo ya operesheni hii maaalum hayatafikiwa mara baada ya wiki sita kumalizika:

Mwitikio wa awali wa kuahirishwa kwa uchaguzi unaonesha kuwa watu wamevunjika moyo na wana mashaka na uamuzi huu. Mgombea u-Rais wa upinzani, Muhammadu Buhari, pamoja na washikadau wakuu wa asasi za kiraia wamewataka watu kuwa watulivu, lakini uamuzi huu umechochea hali ya watu kutokuridhika na hali ilivyo. Mara baada ya kutolewa kwa uamuzi huu, raia wa Naijeria walikusanyika kwenye mitaa ya jiji la Lagos na Abuja kwa ajili ya kufanya maandamano. Kama yangalitokea maandamano ya nchi nzima, kuna maeneo mengi sana ambayo kungeweza kutokea machafuko.

Operesheni hii maalum iliyoanzishwa na jeshi imepangwa kudumu kwa wiki sita. Kumbukumbu ya harakati za kijeshi katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Naijeria kwa miaka sita iliyopita inaonesha uwezekano mdogo kuwa hakutakuwa na mafanikio yatakayoonekana kwa muda huu wa kipindi cha wiki sita. Jambo la kujiuliza ni kuwa, nini kitatokea ikiwa malengo ya operesheni hii hayatakuwa yamekamilika mara baada ya wiki sita kuisha. Jeshi litaomba tena liongezewe mwezi mmoja zaidi? Mwisho wa mwezi Aprili ndio kikomo kwa mujibu wa katiba, hivyo italazimika kwa uchaguzi kufanyika. Au, hata kama haitakuwa vizuri, labda kutakuwa na mapendekezo ya kuundwa kwa serikali ya mpito?

Moyosore Ayodele anajiuliza ni kwa namna gani Boko Haram wanaweza kudhibitiwa ndani ya wiki sita ikiwa ni baaada ya kuendesha matukio ya kigaidi kwa miaka sita:

Kwa miaka 6 haikuwezekana kuwakabili Boko haram, lakini tunataka kuwashinda kwa wiki sita kwa sababu ya uchaguzi. Ni dhahiri PDP=Boko haram.

Ruggedman auliza:

Mikakati ya chaguzi za mwaka 2015 hazikuanza leo, Ni nani aliyepanga muda wa mwezi Februari kwa ajili ya operesheni za kijeshi?

Mtumiaji wa mtandao wa Twita, President Obiang atoa tahadhari kwa kupiga kijembe:

Baada ya miaka mingi, ni jambo jema kusikia kuwa Rais #Goodluck Jonathan anahitaji wiki 6 tu zaidi kukabiliana na Boko Haram.

Kwa mujibu wa Alexander Osondu, kuahirishwa kwa uchaguzi kumekiuka Katiba ya Naijeria:

Uchaguzi ulipangwa kufanyika Machi 28 ni ukiukwaji wa wazi kabisa wa vifungu vya sheria vilivyomo kwenye Katiba ya Nigeria.

Vifungu vya sheria vya katiba vipo wazi kabisa kuhusiana na suala la kuahirishwa kwa chaguzi. S.123(1)

Adaure Achumba, Mwandishi wa habari wa eneo la Afrika ya Magharibi anayeripotia AriseTV, aonesha kutokukubaliana:

Katiba ipo wazi #UchaguziNigeria lazima ufanyike katika kipindi cha siku 90 & na si zaidi ya siku 30 kabla ya Mei, 29. Tarehe 29 Aprili ndio siku ya mwisho kwa mujibu wa sheria.

Hili ni moja ya mambo ambayo baadhi ya watu wanafikiria kuwa limepelekea kuahirishwa kwa uchaguzi:

Anza mapema, kusanya fedha za kutosha ili tuzifuje. Zinapokaribia tu kuisha, ahirisha (Uchaguzi). Wao watakosa fedha( kwaajili ya uchaguzi)

Ryan Cummings, Mchambuzi wa Afrika ya Kusini wa masuala ya Usalama anasema kuwa, kuahirishwa kwa uchaguzi kwa sababu ya Boko Haram ni jambo lisilokuwa na maana kabisa:

Ingekuwa rahisi sana kueleweka kama sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi ingekuwa imesababishwa na matatizo ya usambazaji wa Kadi za Kudumu za wapiga kura (PVC). #BokoHaram siyo sababu yenye mashiko

Hadi wakati ninaandika makala haya, watumiaji wa mtandao wa Twita walishai-twiti na 16 waliipenda Twiti ifuatayo mara baada ya Idhaa ya Sauti ya America ya Hausa kuwaomba watu kutoa maoni yao kuhusiana na kuahirishwa kwa uchaguzi:

SAMBAZA Twiti hii kama hukubaliani na kuahirishwa kwa uchaguzi, IPENDE kama unakubalina na kuahirishwa kwa uchaguzi

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.