Habari kuhusu Kiingereza kutoka Aprili, 2012
Naijeria: Gumzo la Mtandaoni Kuhusu Shirika la Ndege la Dominion
Kwa nini basi kuingia tu kwa jina jipya katika kibiashara ya safari za anga kusababishe majadiliano makali namna hii? Imetokea kuwa shirika hili la ndege si “la kawaida”: linasemekana kumilikiwa na Mtumishi wa injili ya “mafanikio, ” Askofu David Oyedepo.
Bolivia: Wanaharakati Washinikiza Upatikanaji Nafuu wa Mtandao wa Intaneti
Nchini Bolivia, kuunganishwa na mtandao wa intaneti ni miongoni mwa huduma ghali zaidi duniani. Huduma hiyo haina kasi na bado haijaweza kupatikana kwa idadi kubwa ya watu. Kikundi cha wanaharakati kwa kutumia mtandao na nje ya mtandao kinadai huduma nafuu na bora zaidi.
Ajentina: Dokumentari Kuhusu Wenyeji wa Mjini Yatafuta Tafsiri ya Maandishi
Dokumentari iitwayo Runa Kuti iliyoshirikishwa katika mradi wa Haki miliki wa “Creative Commons” kuhusu kutambuliwa kwa wananchi waliotokana na uzao wa wenyeji wa zamani walioishi mjini katika jiji la Buenos Aires, inatafuta watu wa kujitolea kusaidia kuiwekea video hiyo tafsiri ya maandishi kwenda katika lugha za asili za Ajentina kama ki-Quechua, ki-Aymara, -kiMapuche na ki-Guaraní pamoja na ki-Kiingereza.
Uganda: Ndiyo Tunampinga Kony!
Kampeni kwenye mitandao ya kijamii inayokusudia kuongeza uungwaji mkono wa harakati za kumkamata kiongozi wa waasi wa ki-Ganda na mhalifu anayetafutwa kwa udi na uvumba Joseph Kony imechukua sura nyingine.
Bangladesh: Mahakama Yaamuru Kufungwa kwa Kurasa za Facebook kwa Kukashifu Dini
Mnamo tarehe 21 Machi, mahakama moja huko Bangladesh iliziamuru mamlaka zinazohusika kuzifungia kurasa tano za Facebook na tovuti moja kwa kukashifu Mtume Mohamedi, Kuruani na dini nyinginezo. Wanaharakati wa mtandaoni wana hofu kwamba kama amri hiyo itatekelezwa, basi itafungua milango kwa uhuru wa kujieleza kudhibitiwa katika siku za usoni.
Ghana: Matumizi ya Vyombo vya Habari vya Kiraia katika Uchaguzi wa Mwaka 2012
Wananchi wa Ghana wanajitayarisha kwa ajili ya uchaguzi wa rais na wabunge ambao utafanyika tarehe 7 Disemba 2012, Jumuiya ya wanablogu wa Ghana imezindua mradi wa uanahabari wa kijamii ambao una nia ya kufunza wanaharakati, vikundi vya kisiasa na wanafunzi kutumia zana za uanahabari wa kijamii kwa ajili ya kwa ajili ya kuafuatilia na kuripoti shughuli za uchaguzi.
Misri: Kundi la “Muslim Brotherhood” dhidi ya Baraza la Kijeshi – Waonyesha Sura Halisi?
“Maandamano ya watu milioni ya kudai kung'olewa kwa baraza la Ganzouri" ndivyo kilivyosomeka kichwa cha habari cha gazeti rasmi la Freedom and Justice Party kufuatia matukio yaliouacha umma wa Wamisri wakiwa mdomo wazi. Je, nini kimetokea kiasi cha karibia "mvunjiko mbaya" kati ya Baraza la Kijeshi na chama cha kisiasa kilichokuwa karibu kutwaa madaraka, pande ambazo zilikuwa na uhusiano mzuri?
Indonesia: Maandamano ya Kupinga Bei ya Mafuta Yatikisha Majiji
Miji kadhaa ya nchini Indonesia iligubikwa na maandamano na vurugu za kupinga ongezeko la bei ya mafuta ya petroli katika wiki chache zilizopita. Wanahabari za mtandaoni walijadiliana ikiwa ongezeko hilo la bei lilikuwa jambo sahihi. Watumiaji wa Twita waliongeza nguvu ya wavuti wa kublogu ili kurusha taarifa za mapambano kati ya polisi na wanafunzi jijini Jakarta.
Mali: Raia Washtushwa na Mapinduzi ya Kijeshi
Askari walioasi wametangaza kwamba wanatwaa madaraka nchini Mali, baada ya kuwa wameteka nyara kituo cha televisheni ya taifa pamoja na ikulu. Wanadai kwamba serikali ilishindwa kuvipa vikosi vya jeshi la nchi hiyo msaada ili kuwakabili vilivyo wapiganaji wa kabila la Tuareg waliokuwa wakiteka miji ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Tanzania: Mwigizaji Nyota wa Filamu, Steven Kanumba, Afariki Dunia
Tanzania ilimuaga mmoja wa wasanii wake maarufu na nyota wa tasnia ya filamu, Steven Kanumba, kwa maziko yaliyogubikwa na majonzi mazito mnamo tarehe 11 Aprili 2012. Alifariki alfajiri ya Jumamosi, akiwa na umri wa miaka 28, baada ya kile kilichodaiwa kuwa ugomvi wa kimapenzi na rafiki yake wa kike aitwaye Elizabeth Michael kwa jina maarufu “Lulu”.