Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Mapinduzi ya Misri 2011.
“Watu milioni waandamana kushinikiza kung’oka kwa baraza la Ganzouri” ndivyo kilivyosomeka kichwa cha habari cha gazeti rasmi la chama cha FJP (Freedom and Justice Party, yaani Chama cha Uhuru na Haki) kinachohusishwa na kundi la Kiislamu lenye msimamo mkali linalojulikana kama Muslim Brotherhood baada ya matukio yaliyowashangaza watu wengi nchini Misri. Swali la “Ilianzaje?” liliulizwa na kila mmoja. Ni namna gani uhusiano wa karibu kati ya Baraza la Kijeshi la Misri (SCAF) na chama chenye ushawishi mkubwa wa kisiasa usababishe “anguko baya”?
Mfululizo wa tuhuma uliibuka wakati chama cha FJP kilipotoa tamko [ar]:

Sababu zilizotolewa na chama cha FJP kwa kuipinga serikali iliyopo madarakani
-Kuendelea na serikali hii kutaleta wasiwasi kuhusu kutendeka haki wakati wa uchaguzi na kura ya maoni kuhusu katiba
-Je, Baraza la Kijeshi linataka kuharibu lengo la mapinduzi, kuwakatisha watu tamaa, na kuvuruga uchaguzi?
-Baraza la Kijeshi limetishia kuvunja bunge kwa kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Katiba.
-Baraza la Kijeshi kung’ang’ania kuendelea kuiweka madarakani serikali iliyoshindwa itakuwa na maana ya kutaka kuharibu lengo la mapinduzi, kuwakatisha watu tamaa, na kuvuruga uchaguzi
Majibu ya Baraza la Kijeshi yalikuwa na mwelekeo wa kupandisha hasira za watu kama yalivyokuwa matamko ya kikundi cha Muslim Brotherhood, tukikumbuka matukio ya mwaka 1954 wakati kikundi hicho kilipobebeshwa lawama, kupigwa marufuku, kuwekwa kizuizini, na kuteswa na mamlaka za serikali. Baraza limesema kwamba tuhuma za kuvuruga uchaguzi ni uongo mtupu. Walitumia pia sauti yenye vitisho walipotoa wito kwa “kambi fulani za kisiasa” kujifunza kutokana na yaliyopata kutokea.
Umma uliachwa katika hali ya sintofahamu kuhusu nini hasa kitakachotokea katika mchezo huu wa ushindani kati ya watu walioshika madaraka na wale wanaosubiri madaraka. Je, watagongana au ndiyo ilikuwa moja ya vitendo vya mchezo wa kisiasa ambao Misri inautumia siku hizi?
Wakati huo huo, Kikundi hicho cha Muslim Brotherhood kilijaribu kupangilia karata zake, na kutangaza kwamba
Watu wengi walilichukulia jambo hili kuwa ni makosa makubwa, huku wengine wakidai ni dalili za “mwanzo wa mwisho”. Wengine walikitazama kikundi hicho (cha Muslim Brotherhood) kama chama kinachoanza kuchukua sura ya chama cha NDP, ambapo nguvu na fedha vilikuwa kvgezo kvkuu vya kutwaa madaraka.
Watumiaji wa vyombo vya habari vya kiraia wamekuwa wakijipa kazi ya uchambuzi na kutoa maoni na mtazamo wao kuhusu chaguo hili lisilo la kawaida:
Khaled El Baramawy [ar] alimfananisha Shater na Aboul Fotouh (kigogo wa kikundi cha Brotherhood aliyeondolewa baada ya kutangaza nia yake ya kugombea Urais) na akaandika ujumbe huu kwa kejeli kupitia mtandao wa twita:
@Egypress : مره واحد رشح نفسه اتفصل … قام اللي فصله رشح نفسه سبــــــــــــــــحان الله.. يعنى قاله ماعنديش وهو كان عنده جوة ! #Egypt #Ikhwan
Taqadum El Khatib [ar] aliandika kwenye mtandao wa twita:
@Taqadum : الإخوان ..كاذبون كاذبون كاذبون كاذبون كاذبون كاذبون …إلى شباب الإخوان استقيلوا يرحمكم الله واتركوا القيادات الكذابة #ikhwan
Wael Eskaner alikuwa na mtazamo wenye ulinganifu zaidi:
@weskandar: Kama Al-Shater ni mgombea anayekubalika basi Baraza (#SCAF) ni la Ikhwan. Hakuna uwezekano kwamba ndivyo alivyo.blockquote>
Ahmed Aggour aliandika:@Psypherize: Walioonewa wamegeuka na kuwa waonevu #Ikhwan
Hassan El Shater, mmoja wa wana 10 wa Khairat El Shater, hakuwa mwenye furaha sana kufuatia uteuzi wa baba yake alipoandika kupitia mtandao wa twita:
@Hassan_elShater : Ni bahati mbaya baba anagombea Urais!:s
Hakuna ajuaye hitimisho la mchezo huu wa kisiasa unaoendelea nchini Misri, lakini jambo moja ni dhahiri, wa-Misri wanashuhudia kipindi chenye msisimko na ni wao pekee wanaamua historia yao.
Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Mapinduzi ya Misri ya 2011.