Mali: Raia Washtushwa na Mapinduzi ya Kijeshi

Wanajeshi waasi wametangaza kwamba wametwaa madaraka nchini Mali , baada ya kukiteka kituo cha televisheni ya taifa pamoja na ikulu ya nchi hiyo.

Wanadai serikali ya Rais Amadou Toumani Touré imeshindwa kutoa ushirikiano kwa vikosi vyake kijeshi katika mapambano dhidi ya waasi wa Tuareg kaskazini mwa nchi hiyo ambao wanataka kujitenga kutoka nchi hiyo.

Raia wengi wamepatwa na mshtuko iweje mapinduzi yafanyike kipindi cha mwezi mmoja tu kabla ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 29 Aprili, 2012? Bila shaka kulikuwa na nadharia nyingine za kueleza tukio hilo na hatua hiyo ya kijeshi.

Kiongozi wa Mapinduzi nchini Mali Kapteni Sanogo kupitia @Youngmalian

Kapteni Sanogo ndiye kiongozi wa Kamati ya kijeshi ya Taifa ya Kurejesha Demokrasia na Nchi (CNRDR) ambao wanasema wataongoza serikali ya mpito mpaka uchaguzi utakapofanyika.

Msemaji wa kamati hiyo, Lieutenant Kanoré alisema kwamba ingawa wamesimamisha katiba na kuvunja taasisi zilizopo, hawana kusudio la kung’ang’ania madaraka. Mapigano kati ya wanajeshi wanaounga mapinduzi hayo na wale wanaomwunga mkono Rais Toure bado yangali yakiendelea.

Baadhi ya wanasiasa na maafisa wa ngazi za juu wameripotiwa kuwekwa kizuizini mjini Bamako, makao makuu ya nchini hiyo.

Raia wengi wa Mali wameshtushwa kwa kiasi kikubwa na mwelekeo wa matukio. Hapa ni baadhi ya miitikio baada ya kufahamu kuwa wanajeshi waasi walikuwa wametwaa madaraka [fr na ing]:

@TheSalifou: J'ai peur pour mon pays…#Mali

@TheSalifou

@Anniepayep: vraiment! La honte! RT @juliusessoka En Afrique, sortir de l'auberge donne sur les caniveaux. #Mali #PauvrePays

@Anniepayep: Kweli, Aibu RT@juliusessoka barani Africa, mnatoka hotelini kuja kuishia mtaroni #mali

@Abdou_Diarra: Le président malien Amadou Toumani Touré, irait bien et serait « en lieu sûr », selon un militaire loyaliste #Mali

@Abdou_Diarra: Rais wa Mali Amadou Toumani Touré anasemekana kuwa mzima mwenye afya njema na yu mahali salama kwa mujibu wa wanajeshi watiifu #Mali

@Youngmalian: #ATT a été élu démocratiquement par le peuple et son mandat se termine en Juin. de quel droit les militaires agissent au nom du peuple #Mali

@Youngmalian ATT (Rais wa Mali) alichaguliwa kidemokrasia na watu na madaraka yake yalikuwa yaishie mwezi Juni. Wanajeshi wana haki gani ya kuchukua hatua kwa niaba ya watu wa #Mali

@ibiriti: demokrasia haimaanishi tu ni mipangilio ya uchaguzi ili kubadili watu wasio na uwezo na kuwaweka wengine. Ni lazima itoe huduma

@philinthe_: Benki na vituo vya mafuta vilifungwa mjini #Bamako #Mali. Ninaongea na madereva teksi wanataka kulipwa mara dufu ya nauli inayofahamika. Kwenda Sotrama bado ni kati ya sarafu za Mali CFA 100-150

@temite: Chochote kitakachotokea, kitakachoathirika hakikosi kuwa ni umoja, umoja wa kidugu baina ya watu na utamaduni #Mali

Mpango wa siri unaonekana wazi kufuatia mapinduzi kufanyika majuma machache tu kabla ya uchaguzi ambao tayari umeshapangwa [fr]:

@diatus2: le coup d'état était prévisible au #mali car ATT laissant durer la rebellion touareg pour avoir un 3e mandat

@diatus2: Mapinduzi nchini #Mali yalitarajiwa kwa sababu ATT (Rais wa Mali) alikuwa anaruhusu hali hiyo kwa kulea waasi wa Tuareg (wakaazi wa kaskazini mwa nchi hiyo) kwa hiyo alikuwa akijiandalia mapinduzi yeye mwenyewe

@Giovannidjossou: #ATT ne faisait rien contre les #terroristes au nord #Mali car ces troubles lui permettaient de repousser les #élections de juin prochain !

@Giovannidjossou:#ATT (Rais wa Mali) hafanyi chochote dhidi ya magaidi katika eneo la kaskazini mwa Mali kwa sababu (alifikiri) matatizo hayo yangemsaidia kuahirisha uchaguzi mpaka mwakani mwezi Juni!div>

@Joe_1789: JE DENONCE: Le coup d'Etat ourdi par des bandits armés, à la solde de la Françafrique, contre le Mali et son président démocratiquement élu.

@Joe_1789: Ninalaani: Mapinduzi haya ambayo yalipangwa na wanajeshi walioziasi Nchi zizungumzao Kifaransa barani Afrika, dhidi ya Mali na Rais wake aliyechaguliwa kidemokrasia

Ukurasa wa Twita wa Ofisi ya Rais wa Mali haukuwa na taarifa mpya tangu Machi 21 ilipokanusha kuangushwa kwa serikali hiyo [fr]:

@PresidenceMali: Démenti formel : Le Ministre de la Défense n'est ni blessé ni arrêté. Il est à son bureau où il poursuit calmement sa journée de travail

@PresidenceMali: Tamko Rasmi la kukanusha uvumi: Waziri wa Ulinzi hajaumizwa wala kuwekwa kizuizini. Yupo mezani kwake akiendelea na majukumu yake ya kila siku

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.