Tanzania: Mwigizaji Nyota wa Filamu, Steven Kanumba, Afariki Dunia

Mnamo tarehe 10 Aprili, 2012, Tanzania ilimuaga mmoja wa wasanii wake maarufu na nyota katika tasnia ya filamu, Steven Kanumba, kwa maziko yaliyogubikwa na majonzi mazito. Alifariki alfajiri ya Jumamosi tarehe 7 Aprili, akiwa na umri wa miaka 28, baada ya kile kilichodaiwa kuwa ugomvi wa kimapenzi na rafiki yake wa kike, ambaye pia ni mwigizaji, aitwaye Elizabeth Michael kwa jina maarufu “Lulu”.

Kwamba umati zaidi ya watu 30,000 akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal, Mke wa rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete, maafisa waandamizi wa serikali, wasanii na watu wa tabaka mbambali walikusanyika kutoa heshima zao za mwisho katika viwanja vya Leader’s Club vilivyo katika jiji kuu la kibiashara la Dar Es Salaam. Idadi hiyo kubwa inayoingia katika rekodi za pekee ni ushahidi unaothibitisha umaarufu mkubwa wa Kanumba, licha ya kuwa bado na umri mdogo. Katika salamu mbalimbali za rambirambi, mchango wake katika kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania, maarufu kama “Bongo movie”, au pia kama Tollywood kwa kufuata mtiririko wa Holliwood, Bollywood na Norriwood.

More than 30,000 people gathered to pay their last respects. Photo courtesy of @BongoCelebrity.

Zaidi ya watu 30,000 walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho. Picha kwa hisani ya @BongoCelebrity.

Waombolezaji walipiga picha na kutuma ujumbe wa moja moja kupitia mtandao wa twita wakati watu wakiomboleza, ambapo kulikuwa na matukio ya wengine kuzimia [sw] na wengine wakidai kuruhusiwa kulibeba jeneza la mwigizaji huyo nguli aliyetokea kupendwa kuelekea makaburini.

@BongoCelebrity alituma ujumbe kupitia twita [sw]:

@BongoCelebrity: Wananchi wanaimba kwa nguvu wakisema wanataka wamshushe kwenye gari wambebe wenyewe!

Habari za kifo cha Kanumba zilianza kusambaa alfajiri ya Jumamosi kupitia mitandao ya kijamii hususani Facebook na Twita, matumizi ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi, na kisha kudakwa na vyombo vikuu vya habari. Mwanablogu Pretty Sintah aliandika  [sw]:

Dear Wadauzz
nasikitika kutangaza kifo cha Steven kanumba ambaye amefariki leo saa saba ya usiku, maiti ipo Muhimbili hospitali.
Chanzo cha kifo,inasemekana Lulu na Kanumba were dating secretly (walikuwa na mahusiano ya siri), na walikuwa pamoja wakati wa kifo chake,inasemekeana Lulu alimsukuma Kanumba wakiwa katika ugomvi na kanumba akadondoka na kupiga kichwa chini, kitendo kinachosadikiwa kuwa chanzo cha kifo chake. Kwa sasa Lulu yupo Osterbay police (kituo cha polisi Osterbay).
nitawaletea more updates (habari zaidi kadiri nitakavyozipata)
ila tusimlaumu Lulu kwani ugomvi katika mapenzi unatokea.
Angalizo
uki comment (ukitoa maoni yako) naomba ujue nilikuwepo eneo la tukio kuanzia Home (nyumbani) kupeleka maiti hosp na kurudi kwake Sinza,kwa ujumla sijalala,
ni hilo tuu

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=YnZb8hY6Ad8

Mengi yameandikwa kuhusiana na kifo cha Steven kanumba na namna rafiki yake huyo Lulu anavyodaiwa kuhusika (na yaliyotokea), , lakini huenda maoni ya Pretty Sintah aliyoyaweka katika blogu yake yanatoa muhtasari  [sw] wa hisia zinazoonekana kwenye vyombo vya habari vya kiraia kuhusu tukio hili:

It’s so painful to lose you our Hero and the only existed Steven Kanumba ‘the great’. Tanzanians gonna really miss you our best friend. Am sending my condolence to your lovely mom, your young bro, your family members, our bongo movie friends and the entire TZ community.
Its not good to judge anyone on this issue, only God can judge a person, Imagine if you are the one judged by everyone as to what is happening to lulu now!! I am very sure that Lulu was not intending to do any bad thing to Kanumba, and am also sure that Lulu was not involved in this matter in any way, may be there was something else concerning Kanumba's health, but let us wait for the Doctors and Lawyers to play their part.
R.I.P. our beloved Kanumba. It’s a high time for our guys like Vincent Kigosi and others to go on with this good thing Kanumba started; we still have good actors and actresses who can take us to the next level. I really believe in you Ray.

Inauma sana kukukosa ewe shujaa wetu, Steven Kanumba “the great” pekee uliyewahi kuishi. Watanzania watakukumbuka sana rafiki yetu mkubwa. Ninatoa pole kwa mama yako mpendwa, mdogo wako, familia yako, marafiki wa Filamu za Bongo na jamii nzima ya Watanzania.
Si vyema kumhukumu yeyote kwa suala hili, ni Mungu pekee awezaye kumhukumu mtu. Fikiria kama ni wewe ndiye unayehukumiwa na kila mtu kama inavyotokea kwa Lulu hivi sasa! Nina uhakika kwamba Lulu hakukusudia kumfanyia Kanumba yoyote yaliyo mabaya, na nina uhakika kwamba Lulu hakuhusika na tukio hili kwa namna yoyote, huenda kuna kingine kuhusiana na afya ya Kanumba (tusichokijua), lakini hebu tusubiri Madaktari na Wanasheria wafanye kazi yao.
Pumzika kwa Amani mpendwa wetu Kanumba. Ni wakati muafaka kwa watu wetu kama Vincent Kigosi na wengine kuendeleza kitu chema alichokianzisha Kanumba; bado tuna waigizaji wazuri wanaoweza kutupeleka kwenye hatua nyingine ya juu zaidi. Ninakuamini sana Ray.

Wavuti ametengeneza ukurasa maalumu wa kukusanya habari kutoka vyombo vya habari vya kiraia [sw] pamoja na ujumbe wa mwisho katika mtandao wa twita alioutuma Kanumba, pamoja na zile zilizotumwa na mashabiki wake baada ya kifo chake.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.