Habari kuhusu Kiingereza kutoka Oktoba, 2014
Wakati Taiwani Ikifikiria Usawa wa Haki ya Ndoa, Maelfu Wahudhuria Matembezi ya Mashoga
Matembezi ya watu wenye mapenzi ya jinsia moja yamefanikiwa mwaka huu huko Taiwani. Wapenzi wawili mashoga katika hali ya kujawa matumaini walivaa fulana zenye ujumbe kuwa wanajiandaa kuoana
Jiandikishe Sasa kwa Mkutano wa Global Voices 2015: Januari 24-25 jijini Cebu, Ufilipino
Jiandikishe sasa kwa ajili ya Mkutano wa Global Voices 2015 jijini Cebu, Ufilipino, utakaokusanya wanaharakati na waandishi wa kiraia kutoka duniani kote.
Miaka 50 Baadae, wa-Zambia Wanajiuliza Nini Maana ya Uhuru
Wakati wa-Zambia duniani kote wakisherehekea siku kuu hiyo kwa vyakula, rangi rasmi za nchi hiyo na chochote walichoweza kukifanya, baadhi ya wachunguzi wa mambo waliibua maswali mazito kuhusu historia na mustakabali wa nchi hiyo.
Salamu ya ‘vidole vitatu’ Yaleta Matumaini kwa Wanaharakati wa Demokrasia Nchini Thailand
Wahudhuriaji wa mazishi ya afisa wa zamani wa serikali walionesha ishara ya vidole vitatu ambayo inatumiwa na wanaharakati wanaopigania demokrasia nchini Thailand.
‘Uandishi na Vyombo vya Habari Katika Kuleta Dunia Bora Zaidi': Mkutano wa Taasisi ya Transformational Media 2014 Jijini DC
Washiriki wa Mkutano wa TM watajadili uandishi, ubunifu, teknolojia mpya, bishara na maisha enedelevu, ustawi na afya, upigaji picha, filamu na muziki,uandishi wa habari, pamoja na mambo mengine
Pamoja na Tishio la Ebola, Waafrika Magharibi Waendelea Kutulia na Kuikumbusha Dunia Wao Ni Nani
Wakati Vifo vinavyookana na Ebola vinakaribia 5,000 huku wagonjwa walioripotiwa wakifikia 10,000 wananchi wa Afrika Magharibi watumia nguvu ya mitandao ya kijamii kupambana na ugonjwa wa Ebola
GV Face: ‘Tupige Kura au Tusipige'? Sauti za Raia wa Tunisia Katika Uchaguzi Unaokaribia
Zaidi ya wagombea 9,000 wa vyama zaidi ya 100 wanagombea kwenye uchaguzi wa mwaka huu
Wanablogu wa Brazili Wadai Mgombea Urais Anawadhibiti Wakosoaji wake Kwenye Mtandao wa YouTube
Watumiaji wenye majina na historia inayofanana wamedai haki miliki dhidi ya video mbili za You Tube zinazomkosoa Mgombe Urais wa Brazili Aécio Neves.
GV Face: Mazungumzo na Mwanaharakati wa Bahrain Ambaye Bahrain Isingependa Tumsikie
Bahrain imeingia mwaka wa tatu ya mapambano na wanaharakati. Taarifa za vyombo vya habari vya Kimataifa zinadai maandamano hayo ni mapinduzi yanayoongozwa na Shia dhidi ya utawala wa Sunni, lakini wanaharakati wanasema hayo ni maelezo mepesi.
Hukumu ya Haki? Ina uzito wa Kutosha? Oscar Pistorius Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Mitano Jela
Mkimbiaji wa Afrika Kusini aliyepatwa na hatia kwa kumwuua pasipo kukusudia rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp imelinganishwa na hukumu ya jangili aliyefungwa miaka 77 jela kwa kumwuua faru mwezi Julai