Habari kuhusu Kiingereza kutoka Septemba, 2013
VIDEO: Shairi la Filamu “Maombi ya Woga” Latia Fora Misri
Mkusanyiko wa kiraia la Misri Mosireen umekuwa, bila kuchoka, ukiweka kumbukumbuza Mapinduzi ya Januari 25 na matukio yaliyofuata baadae kwa kutumia picha na dokumentari. Moja ya ubunifu wake wa mwisho mwisho ni “Maombi ya Woga”, shairi la filamu iliyotengenezwa na Mahmoud Ezzat na kusimuliwa na mwanachama wa Mosireen Salma Said....
South Korea: Ahadi ya Rais ya Ustawi Iliyoshindwa Yakosolewa
Rais Park yuko kwenye wakati mgumu kwa r ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni kuwa angepandisha ruzuku ya pensheni gharama za mafunzo. Wakosoaji wanasema kampeni yake iliahidi kinyume na sera yake kama mgombea mhafidhina, ilimsaidia kuzoa kura katika uchaguzi uliopita. Akaunti ya mtandao wa twita wa @metempirics ilikusanya viunganishi vinavyohusika na...
Boko Haram Waua Wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu Nchini Naijeria
Kikundi cha kigaidi cha Naijeria Boko Haram kimewawasha moto bwenini na kuwaua wanafunzi wasiopungua 50 wa Chuo Kikuu cha Kilimo kilichopo kwenye Jimbo la Yobe, wakiwa usingizini. Rais Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika eneo hilo kufuatia mfululizo wa vitendo vya kigaidi.
India: Mgombea wa Uwaziri Mkuu na Historia yake ya Uhalifu
“Je, mtu anaweza kuwa na historia ya uhalifu na bado akawa Waziri Mkuu wa India?” – anauliza Dr. Abdul Ruff wakati anajadili uteuzi wa kiongozi wa mrengo wa kulia na Waziri Mkuu wa Gujarat Narendra Modi. Ni mgombea wa Uwaziri Mkuu wa chama cha National Democratic Alliance katika uchaguzi mkuu...
Bhutan: Sheria za Uchaguzi Zahitaji Mabadiliko
Yeshey Dorji anaunga mkono hatua ya Baraza la Taifa Butan kuanzisha mjadala wa rushwa wakati wa uchaguzi ambazo zimeripotiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita zinazohitaji marekebisho yanayowezekana ya sheria ya uchaguzi.
Kwa nini Indonesia Haitakiwi Kupandisha Kima cha Chini cha Mshahara
Rocky Intan aneleza kwa nini kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara nchini Indonesia kutaathiri uchumi wa nchi hiyo: Viongozi wa kitaifa na wale wa ngazi za chini lazima wapambane na shinikizo la baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakzi wanaodai kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara. Ongezeko la...
GV Face: Magaidi Wanatwiti? Shambulio la Westgate
Toleo la juma hili la mfululizo wa Mazungumzo yetu ya GV Face kupitia Google Hangout, tunajadili wajibu wa uandishi wa kiraia baada ya tukio la kigaidi la Kenya.
Picha Nyeusi: Waafrika Nchini Italia
Picha Nyeusi ni kazi za wapiga picha watatu – Marco Ambrosi, Matteo Danesin na Aldo Sodoma – Kituo cha Stadi za Uhamiaji mjini Verona, Majiji ya Verona na Padua, Chuo Kikuu cha Padua Idara ya Sosholojia ikiwaonyesha Waafrika nchini Italia.
GV Face: Mitazamo Tofauti Kuhusu Habari za Mgogoro wa Syria
Namna gani taarifa za Syria zinatofautiana kulingana na uliko? Na hilo linamaanisha nini kwa wananchi wa Syria? Tulilizungumza hili pamoja na mambo mengine katika toleo la pili la GV Face.
Shambulizi la Nairobi Lasababisha Kutengenezwa kwa Zana Mbili za Dharura Mtandaoni
Zana tumizi ya "The Ping" itawasaidia wanafamilia kutafutana haraka wakati wa dharura wakati "Blood Donation Kenya" itasaidia kuoanisha vituo vya utoaji damu na watu wanaojitolea damu.