GV Face: Mitazamo Tofauti Kuhusu Habari za Mgogoro wa Syria

Ni namna gani habari zinazozungumzia mgogoro wa Syria zinategemeana na mahali uliko? Na hiyo ina maana gani kwa raia wa Syria?

Tulijadili suala hili na mengine mengi kwa kutumia zana ya majadiliano ya Google Hangout Jumatatu ya Septemba 23, 2013, saa 3 alasiri UTC katika toleo letu la pili la GV Face.

Taarifa katika nchi za Marekani au Uingereza zinadai kuwa silaha za maangamizi zilitumiwa na utawala wa Rais Assad kuwaua watu zaidi ya elfu moja nchini Syria mwezi uliopita. Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Urusi vinasema, “hali ni shwari” mjini Damascus. Vyombo vya Habari vya Iran vinadai shambulio la kemikali lilifanywa na “waasi” katika juhudi za kutaka kuongeza shinikizo la kimataifa kuingilia kati.

Wakati serikali ya Marekani ifikiri kuishambulia Syria kijeshi, Rais wa Urusi akiwa New York amewasihi watu wa Marekani kufutilia mbali mpango wao wa kuipiga nchi hiyo ambayo tayari imeshaharibiwa mno na vita. Video zinazoonyesha dalili ya hatua za kijeshi zinazochukuliwa na Iran nchini Syria zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Washiriki wa mazungumzo yetu hayo ya mtandaoni walikuwa ni pamoja na mwandishi wa Gv Syria, Leila Nachawati, Mwanzilishi wa Syria Untold, mradi wa kupashana habari mtandaoni uliojikita kwenye mapinduzi ya amani yanayofanywa na wananchi wa Syria; Mhariri wetu wa RuNet Echo Kevin Rothrock aliyezungumza kuhusu Putin na Mc Cain OpEds na namna wanavyotazamwa na mitandao ya Urusi; Amira Al Hussaini, Mhariri wetu wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, aliyegusia habari zilizikuwa zinaandikwa na vyombo vya habari vya kiraia na vyombo vikuu vya habari ndani ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini; Solana Larsen, Mhariri Mtendaji alizungumzia kuhusu wajibu wa vyombo vya habari vya kiraia katika taswira inayojengwa na vyombo vikuu vya habari kuhusu Syria, Ellery Biddle Mhariri wa Utetezi aliyezungumza namna wito wa kuiomba Marekani kuingilia kati mgogoro huo inavyotafsiriwa na raia wa Marekani mtandaoni na Ivan Sigal Mkurugenzi Mtendaji aliyetoa maoni yake kuhusu namna habari za Syria zinavyoumbwa kuwa vile zilivyo duniani kote.

Kupata habari za kimataifa zilizojikita kwenye Mgogoro wa Syria, unaweza kupitia ukurasa wetu maalumu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.