GV Face: Magaidi Wanatwiti? Shambulio la Westgate

Mitandao ya kijamii imefanya kazi kubwa katika kusambaza habari za shambulio la kigaidi lililofanyika kwenye jengo la Westgate, Nairobi, Kenya, lakini hata hivyo taarifa hizo zisizothibitishwa zilisambaa mithili ya mwale wa radi, iwe ni kutoka serikalini, kwa magaidi wenyewe, waandishi wa habari na hata raia wa kawaida katika mitandao ya Facebook na Twitter.

Je, hili linatupa ujumbe gani kuhusu utafutaji wa habari za kweli baada ya shambulio hili la kutisha dhidi ya raia wa Kenya?

Je, yanayotangazwa na vyombo vikuu vya habari yana maana yoyote, kama yeyote anayetaka kupata habari halisi anatafuta alama habari kwenye mtandao wa twitter?

Siku ya Ijumaa, Septemba 27, 2013, timu ya Global Voices ya Kusini mwa Jangwa la Sahara – Omar Mohamad  na Collins Mbalo  walijibu maswali haya na mengine mengi kwenye mfululizo wa Mazungumzo yetu ya Gv Face yaliyofanyika kwa kutumia zana ya Google Hangout. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.