Habari kuhusu Kiingereza kutoka Septemba, 2013
Waziri wa Uganda: Wanawake Wasiovaa Mavazi ya Heshima Wanaomba Kubakwa
Waziri wa Mambo ya Vijana wa Uganda Ronald Kibuule ametakiwa kwenda bungeni kujieleza kuhusiana na matamshi yake ya hivi karibuni
Uvumi Waenea Kwamba Putin Amefunga Ndoa Nyingine
Kumekuwepo na tetesi za muda mrefu kuwa Putin ana uhusiano wa kimapenzi na mcheza sarakasi Alina Kabaeva. Uvumi umekuwa mkubwa, kiasi cha kuhisiwa kuwa "wapenzi" hao hatimaye wameoana.
Vyombo vya Habari vya Magharibi na Taswira ya Ellen Sirleaf Johnson
Aaron Leaf anajadili jinsi taswira ya rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, hujengwa na vyombo vya habari kimagharibi kama alama ya mambo yote mazuri. Anasema kwamba hili ndiyo simulizi lililomwezesha Sirleaf kuwa mhimili wa maendeleo ya kimataifa na uwezeshaji wa wanawake.
Mwandishi wa Global Voices Awakumbuka Marafiki Waliouawa Kwenye Shambulio la Nairobi
Shurufu, mwandishi wa Tanzania anayeishi Dar es Salaam, alipoteza marafiki Ross Langdon na Elif Yavuz, waliokuwa wakimtarajia mtoto wao wa kwanza.
Blogu na Uhuru wa Saudi Arabia
Saudi Arabia inasherekea Siku ya Uhuru tarehe Septemba 23. Wanablogu wanaeleza matumaini yao kwa taifa ambalo linaheshimu na kuthamini watu wake na matarajio yao.
Bunge la Tanzania Lageuka Uwanja wa Masumbwi
Siku za hivi karibuni, Mbunge wa Bunge la Tanzania alijikuta katika wakati mgumu pale alipokabiliana kwa nguvu na majibizano na maafisa wa usalama wa Bunge. Si mara ya kwanza kwa hali ya mambo kuishia kwa machafuko katika Bunge la Tanzania.
Kubusiana Kwenye Mitaa ya Misri
Picha inayosambazwa katika mtandao wa Facebook inayowaonyesha vijana wawili raia wa Misri wakibusiana barabarani iliibua hasira na wengine kuipenda. Ilitolewa na Ahmed ElGohary, mtangazaji aliyepingwa kwa ‘kukosa utu uzima’ kwa sababu ya kuweka picha ya jinsi hiyo. Wengine walisifu uzuri wa picha hiyo na tafsiri yake kwa mapinduzi ya kiutamaduni. Kuonyesha mapenzi hadharanini si jambo linalokubalika nchini...
Vumbi la Uchafuzi wa Mazingira Larudi Nchini Indonesia
Vumbi linalosababishwa na uchafuzi wa mazingira ni tatizo la mara kwa mara katika eneo hilo linalosababishwa zaidi na matukio ya moto wa msituni nchini Indonesia.