Mwandishi wa Global Voices Awakumbuka Marafiki Waliouawa Kwenye Shambulio la Nairobi

Shurufu ni mwandishi wa Tanzania anayeishi Dar es Salaam. Anatwiti kupitia@shurufu. Pia waweza kusoma posti yake Namna shambulizi la Westgate jijini Nairobi lilivyobainikia kupitia Mitandao ya Kijamii.

Wakati wa kuandikwa kwa posti hii, idadi ya watu waliouawa katika shambulizi la kikatili kwenye kituo cha kibiashara jijini Nairobi ilifikia 69, wakati wengine 200 wakijeruhiwa. Wanajeshi wenye silaha walivamia jengo hilo, moja wapo ya maeneo maarufu zaidi jijini humo linalotembelewa na raia wa kigeni na wa-Kenya wa tabaka la kati, na kufanya shambulizi la kikatili zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu kulipuka kwa bomu katika jengo la Ubalozi wa Marekani mwaka 1998.

Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na Mshairi anayeheshimika, raia wa Ghana Kofi Awoonor. Mwingine ni mtangazaji maarufu, Ruhila Adatia. Inasemekana alikuwa mjamzito.

Mimi, vilevile, nimepoteza marafiki katika shambulio hilo la Westgate: Ross Langdon na Elif Yavuz, wenzi waliokuwa wakimtarajia mtoto wao wa kwanza. Waliishi Dar es Salaam lakini walikuwa Nairobi kwa ajili ya kujifungua kwa sababu ya kuziamini zaidi huduma za afya jijini humo. Elif alimaliza PhD yake katika Shule ya Afya ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Harvard. Alihamia Dar es Salaam kufanya kazi katika Mfuko wa Clinton. Hapa chini, akikutana na Rais Bill Clinton wakati wa ziara yake nchini Tanzania mwezi Agosti:

Elif Yavuz meeting with President Bill Clinton during his visit to Tanzania in August

Elif Yavuz akikutana na Rais wa zamani Bill Clinton wakati wa ziara yake nchini Tanzania mwezi Agosti 2012. Picha kupitia ukurasa wa Facebook wa Yavuz .

Elif alikuwa na akili, anayejua kutumia maneno vizuri, mchezi na mtu wa kufurahia kuwa nae. Angekuwa mama mwema ajabu. Rafiki yake wa kiume Ross alikuwa na bashasha na ucheshi wa ki-Australia na mwenye furaha ya maisha kama ilivyo kawaida ya watu wakarimu na wanyenyekevu kutoka Australia. Alikuwa mbunifu wa majengo mwenye kipaji cha ajabu. Alishiriki kuanzisha kituo cha kimataifa cha ubunifu wa majengo, kinachooitwa Regional Associates. Hapa anazungumzia kile alichokiita ubunifu wa Kinyonga katika mkutano wa TEDxKraków wa mwaka jana:

Alikuwa akitarajia kuwa Baba.

Lakini Ross na Elif wametutoka. Ni vigumu kueleza kwa nini watu hawa wema ajabu kiasi hiki pamoja na Profesa Awoonor na Bi. Adatia, wakiwa na Mbugua na Wahito na roho zote zisizo na hatia zilizopotea katika Shambulio la Westgate.

Katika maneno ya mwandishi Teju Cole (@tejucole), mroho zao zipumzike kwa amani katika ulimwengu mpya.

Soma pia: Namna shambulizi la Westgate jijini Nairobi lilivyobainikia kupitia Mitandao ya Kijamii.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.