Bangladesh: Mahakama Yaamuru Kufungwa kwa Kurasa za Facebook kwa Kukashifu Dini

Mnamo tarehe 21 ya Mwezi Machi, 2012, mahakama ya Bangladesh iliamuru mamlaka zinazohusika kuzifungia kurasa za mtandao wa Facebook na tovuti moja kwa kumkufuru Mtume Mohammad, Koran na imani nyingine za kidini. Hukumu hiyo imehoji kwa nini wamiliki/watengenezaji/waendeshaji wa tovuti/kurasa hizo wasipelekwe mbele ya sheria kwa kupandisha mtandaoni maudhuri yasiyo na nidhamu ya kimaadili. Kinacholeta wasiwasi zaidi ni kwamba amri hiyo inahoji kwa nini mchakato kama huo wa kuzifunga tovuti/kurasa kama hizo katika siku za usoni usianzishwe.

Awali, wahadhiri wawili wa Chuo Kikuu walifungua kesi wakilalamika kwamba kurasa hizi na tovuti hiyo zilikuwa zinaleta usumbufu wa hisia za kidini kwa watu. Facebook ni mtandao ulio maarufu sana nchini Bangladesh na kwamba watumiaji wanaokadiriwa kuwa milioni 2.5 huku nchi hiyo kwa ujumla ikishika nafasi ya 55 duniani. Mwaka 2010 mtandao wa Facebook ulizuiwa kwa muda kufuatia mashitaka ya propaganda chafu dhidi ya Waziri Mkuu zilizodaiwa kusababisha usumbufu wa hisia za kidini kwa watu.

block Facebook Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kurasa zilizotuhumiwa zina maoni na katuni tofauti kuhusu Mtume Mohammad, Koran kitabu Kitakatifu cha Waislam, Yesu, Bwana Buddha na miungu ya ki-Hindu. Baadhi ya katuni za miungu zinasemekana kuwa karibu sana na picha za ngono.

Raia watumiao mtandao walichukua muda kuanza kuzungumzia suala hili kwa kujua kuwa palikuwa na shitaka dhidi ya mhadhiri wa Chuo Kikuu kufuatia kile alichokuwa amekiweka kwenye ukurasa wake. Kama vile haitoshi, kuna shinikizo kwa serikali kufuatilia kwa karibu yote yanayoendelea katika mtandao wa Facebook kwa sababu ya kile kinachoonekana kwamba (mtandao huo) unaweza kutumika kwa makusudi yoyote. Aidha, watumiaji hao pia walikuwa na wasiwasi ikiwa hukumu hii, kama itatekelezwa, itatumika kuhalalisha kubanwa kwa uhuru wa kujieleza mtandaoni.

Tanvir, mtumiaji wa mtandao wa Facebook aliuliza kwa angalizo: [bn]:

সংবিধানের ২৭ অনুচ্ছেদঃ সকল নাগরিক আইনের দৃষ্টিতে সমান এবং আইনের সমান আশ্রয় লাভের অধিকারী।

দেশে হিন্দু / বৌদ্ধ / খ্রিস্টান / নাস্তিক / মুক্ত-মনা / সংশয়বাদী / Agnostik ইত্যাদি দের সংখ্যা কম বিধায় তাদের অনুভুতি কম মূল্যবান এবং মুসলমানরা বেশি বিধায় তাদের অনুভুতি বেশী মূল্যবান এরকমটা আদালত মনে করেন কিনা জানতে চাই।

Ibara ya 27 ya katiba: Kila raia ni sawa mbele ya sheria na sheria inamlinda kwa usawa.
Ninataka kujua ikiwa mahakama tukufu inataka tuamini kwamba waumini wa dini za Kihindu/Kibudha/Kikristo/wasioamini uwepo wa Mungu/wapagani/wanafalsafa na kadhalika ni wachache sana nchini (Bangaldesh) kwa hiyo hisia zao hazina umuhimu wa kutosha na kwamba kwa kuwa tunao Waislamu wengi basi hisia zao ni za muhimu zaidi ya waumini wengine.

বিজ্ঞ আদালত শুধু ধর্মানুভুতিতে আঘাত থামাতে আগ্রহী নাকি সব ধরণের অনুভুতিতে আঘাত থামাতে আগ্রহী (উদাহরণস্বরূপঃ আদালতানুভুতি, বিজ্ঞানানুভুতি , ইতিহাসানুভুতি, ক্রীড়ানুভুতি)…ইদানীংকালে আমরা অনেক ধরণের অনুভুতিতে লোকজন কে আঘাত হানতে দেখি । বড়ই অনুভুতি পরায়ণ জাতি এই বাঙালি।

Ikiwa mahakama tukufu inataka kulinda watu wasipate bughudha ya hisia zao kidini au hisia nyingine pia (mfano hisia za hukumu za kimahakama, hisia za sayansi, hisia za historia, hisia za michezo nk)…tunaona kwamba watu wanabugudhi kila aina ya hisia za watu wengine wasioamini kama wao. Sisi Wabangladesh tunaonekana kuwa na hisia sana na hisia zetu.

Tanvir anatoa maoni:

কিন্তু ধর্মকে অবান্তর ব্যাঙ্গ বিদ্রুপ আর কটূক্তি অনুসরণযোগ্য না হলেও এই কাজগুলো বন্ধের চেষ্টায় ফোরাম /ব্লগ / ওয়েবসাইট বন্ধ করে দেয়ার বিজ্ঞ আদালতের সিধান্ত কোন ভাবেই সমর্থনযোগ্য নয় কেননা এতে করে যৌক্তিক ও বস্তুনিষ্ঠ সমালোচনার পথ ও রুদ্ধ করা হয় ।
মনে রাখতে হবে , কলমের জবাব সবসময় কলম দিয়েই দেয়া উচিও, তলোয়ার বা পেশিশক্তি দিয়ে নয়।

Ninapinga kabisa kejeli na maigizo yasiyo ya msingi kwa dini za watu lakini siwezi kuunga mkono hatua za kufunga Majukwaa ya mijadala/blogu/tovuti kama hatua za kuzuia kejeli hizo. Kwa sababu kufanya hivyo husababisha moja kwa moja kufungwa kwa majukwaa ya mijadala yenye kujenga na yenye kimantiki.
Ni lazima tukumbuke, jibu la kalamu hutolewa kwa kalamu, na sio kwa kutumia upanga au misuli.

Watumiaji wengine wa Facebook wanaunga mkono kufungiwa huko huku wanakumbusha kwamba kuna tovuti kadhaa zinazoendeshwa na watu waukanao uwepo wa Mungu nchini Bangladesh ambazo hazina maudhui ya kashfa isipokuwa hoja kinzani zenye kujenga. Hukumu ya hivi karibuni haikuwa dhidi ya tovuti hizi bali zile ambazo kwa kweli zinaharibu.
Mtumiaji mwingine wa Facebook aitwaye Ranadipam anasema:

কোন অন্তর্জালিক সাইটের নৈঃশব্দ আমাকে বিরক্ত বা ডিস্টার্ব করে না। ওগুলোতে ঢোকা বা না-ঢোকার স্বাধীনতা রয়েছে আমার। কিন্তু আশেপাশের আয়োজিত ধর্মসভা এবং অন্যান্য আয়োজনগুলোর কানফাটানো মাইকের চিৎকার আমি না-চাইলেও আমার ব্যক্তিস্বাধীনতা বিপন্ন করে আমাকে বিরক্ত করে। আমার সবরকমের অনুভূতিকে আঘাতপ্রাপ্ত করে। এর প্রতিকার আমি কার কাছে চাইবো ?

Kuzinyamazisha tovuti hizo hakunighasi kwa sababu nina haki ya kuingia au kukwepa tovuti zinazohusika. Lakini mawaidha ya kidini na hata sauti kubwa zinazotokana na ibada za dini nyingine hapa nilipo kwa kweli zinaingilia haki zangu binafsi na kunisumbua. [Kelele hizo] zinabughudhi kila aina ya hisia ninazoweza kuwa nazo. Ninapata wapi haki?

Mamlaka zinazohusika zimesema kwamba zimewasiliana na uongozi wa (kampuni ya) Facebook kwa minajili ya kuzifungia kurasa hizi na raia wa Bangladesh watumiao mtandao wana bahati kwamba wakati huu mamlaka zinaheshimu na kutekeleza amri ya mahakama kwa makini na hakuna kufungiwa kwa mtandao wa Facebook kunafanyika kwa maneno matupu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.