Habari kutoka na

Mwaliko wa Mapendekezo ya Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2014

  30 Januari 2014

Waandaaji wa Tuzo za Blogu nchini Kenya 2014, ambao ni Umoja wa Wanablogu nchini humo (BAKE) kwa sasa wanakaribisha mapendekezo ya wawaniaji wa tuzo hizo mpaka Februari 10, 2014.  Watumiaji wanaweza kupiga kura kwa njia ya mtandao kuanzia Machi 1, mpaka April 30, 2014 kupendekeza blogu wanazoona kuwa ni bora...

“Nchi” Nzuri ya Afrika

  11 Novemba 2013

Katika toleo la wikii hii la Brainstorm, jarida la mtandaoni la Kikenya, Brenda Wambui hulaani masimulizi ya sasa kuhusu Afrika: “Afrika ni nchi”, “Afrika inapaa”, ‘”Mitindo ya Kiafrika.” Huchunguza jinsi Wakenya wanavyoweza kukomboa simulizi lao na kujiainisha kwa kuweka masharti yao wenyewe: Kama wenyeji wa Kenya ama nchi nyingine ile,...

Fuatilia SafariYaGariAfrika Mtandaoni

  7 Oktoba 2013

Kikundi cha watengenezaji na wabunifu wa teknolojia kutoka Ulaya ambao wanadadisi ukuaji wa vituo vya teknolojia barani Afrika wanaendelea na safari yao ya gari barani humu. Tazama blogu yao au Tumblr na ufuatilie mjadala kuhusu safari yao kwenye mtandao wa Twita.

Mwenendo wa Mashitaka ya Wanasiasa wa Kenya Mjini Hague

  7 Oktoba 2013

Mashitaka ya Kenya Hague ni mradi wa Dawati la Afrika la Radio Netherlands Worldwide kwa ushirikiano na This is Africa (Hii ni Afrika): Namna gani ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 na 2008 ziliathiri maisha yako? Unataka kufahamu nini kuhusu haki ya kimataifa? Changia habari ulizonazo, mawazo...

Daktari wa Peru ni Miongoni mwa Waathirika Waliopeza Maisha Westgate

  27 Septemba 2013

Shirika la Habari la Andina limearifu [es] siku ya Jumamosi, Septemba 21, 2013, kwamba daktari wa ki-Peru Juan Jesús Ortiz ni mmoja wa watu waliuawa katika shambulizi la kigaidi lililotokea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, lilisababisha idadi ya vifo vya watu 59 na wengine 175 wakijeruhiwa. Hivi ndivyo Periodismo...

Blogu 10 Bora za Mapishi ya ki-Afrika

  11 Februari 2013

MyWeku anatengeneza orodha ya Blogu 10 bora za Mapishiya ki- Afrika kwa mwaka 2013: “Inaonekana kuna blogu milioni moja zinazozungumzia mapishi, lakini ni chache sana zinazoonyesha vyakula vya Kiafrika. Pamoja na hayo imekuwa kazi ngumu kuchagua 10 kati ya nyingi nzuri kwa mwaka huu 2013.”

Jukwaa la Kiafrika Lenye Makala za Bure za Kitaaluma

  22 Januari 2013

Januari 24, ni siku ambayo inategemewa kuwa ya kuzindua rasmi Hadithi, ambalo ni jukwaa la kuhifadhia zana za bure za kitaaluma mjini Nairobi, Kenya. Wasomi mbalimbali na wadau wa mitandao watakusanyika pamoja kujadili upatikanaji wa zana huru za kitaaluma katika elimu ya juu nchini Kenya. Hadithi itasaidia kutafuta, kuona na kushusha...

Kenya: Kiswahili Kuwa Somo La Kuchagua

  22 Januari 2010

Bunmi anaandika kuhusu uamuzi wa kulifanya somo la Kiswahili kuwa la kuchagua nchini Kenya: “Somo hili halitakuwa tena na mtihani wa lazima katika mtihani wa taifa wa darasa la nane…”