Wasanii wa Brazil Waungana Kuwahifadhi Simba Nchini Kenya

Leo Vultus by Murillo Martinsfor the campaign Run4Run4Lions.

Leo Vultus kwa niaba ya Murillo Martins kwa kampeni ya Run4Run4Lions.

Baada ya uchapishaji wa pamoja #sobreontem (kuhusu jana) katika kusaidia harakati [pt] ambayo ilianzishamaandamano haya Juni iliyopita mjini São Paulo, wasanii wa Brazil sasa wanajiunga pamoja kwa sababu mpya. Wakati huu, kazi yao ni dhidi ya kuuawa kwa simba katika mkoa wa Samburu, Kenya.

Wenyeji wa mkoa wanatumia sumu na silaha nyingine dhidi ya simba ambao huwashambulia mbuzi wao. Kuongeza kuelewa kwa umma kuhusu suala hili, katika mwaka 2010 Mradi wa Ewaso wa Simba uliandaa mbio za nusu-marathon kwa lengo la “kutuliza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori kwa kushirikisha jamii katika uhifadhi wa simba.” Kwa waandaaji, sehemu ya ufumbuzi wa tatizo ni “mbuzi za bure zaidi”, na ni kwamba katika tukio la kwanza mwaka 2010, zawadi ya kushinda mbio walikuwa mbuzi.

Sasa mradi unafanya maandalizi ya mashindano ya pili na kampeni crowdfunding #Run4Run4Lions, ambayo itakusanya fedha kwa ajili ya mbio za nusu-marathon mwaka wa 2014. Michoro ya awali ya Wasanii wa Brazil (ambayo baadhi ya vipande tayari vimeuzwa) inayotolewa kama fidia kwa wale ambao wanasaidia mradi.

Kujifunza zaidi kuhusu kampeni

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.