Habari kuhusu Mahusiano ya Kimataifa kutoka Julai, 2013
Maandamano ya Kudai Uchaguzi nchini Madagaska Yasababisha Vurugu
Blogu ya Vola R ya Ma-Laza inaandika kwamba watu 7 walijeruhiwa [fr] kufuatia matumizi ya nguvu yaliyofanywa na polisi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanadai kufanyika kwa uchaguzi mjini Antananarivo, Madagaska. Chama...
Hali ya Kidiplomasia Kati ya Zimbabwe na Nchi za Magharibi
Simukai Tinhu, mchambuzi wa masuala ya siasa anayeishi London, anauliza, “Je, mahusiano ya Zimbabwe na nchi za kimagharibi yanaimarika kadri uchaguzi unavyokaribia?”
Je, Ziara ya Obama Barani Afrika ni Neema au Hasara?
Rais wa Marekani Barack Obama amemaliza ziara yake ya siku sita katika nchi tatu za Kiafrika, Senegali, Afrika Kusini na Tanzania, mnamo Julai 2, 2013. Obama alitangaza mradi mpya, "Umeme Afrika", kukuza matumizi ya umeme mara dufu katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara. Maoni ya watu duniani kote juu ya umuhimu na matokeo ya ziara hiyo yamegawanyika mno.
Obama Barani Afrika: Vita ya Kibiashara na China?
Rais Obama ametembelea bara la Afrika kwa ziara iliyokuwa imepangwa kati ya tarehe 26 mpaka Julai 3, 2013. Hivi karibuni alikuwa nchini Afrika Kusini baada ya kutembelea Senegali na baadae aliitembelea Tanzania. Wachambuzi wengi wanaoiona safari hiyo kama mpango wa kushindana , kama jaribio la Marekani kupambana na mafanikio ya kiuchumi ya China katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Watanzania Waitafakari Ziara ya Obama Iliyosubiriwa kwa Matumaini Makubwa
Dar es Salaam, ambao ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania, unarejea katika hali yake ya kawaida baada ya siku mbili za kuwa mwenyeji wa mtu anayeaminika kuwa mwenye mvuto mkubwa duniani, Rais wa Marekani, Barack Obama. Mitaa ya jiji la Dar Es Salaam ilihanikizwa na picha za Rais huyu.