Habari kuhusu Mahusiano ya Kimataifa kutoka Agosti, 2012
Kocha wa Timu ya Taifa ya Zambia Atunukiwa Ukaazi wa Kudumu
Zambia imewahi kuwa na makocha wengi wa kigeni wa timu ya Taifa ya soka, lakini ni Mfaransa Herve Renard, aliyeongoza timu hiyo hadi kushina Kombe la Washindi Barani Afrika mwaka 2012, aliyepata upendeleo wa pekee. Ili kutambua mafanikio yake haya, serikali imemtunuku ukaazi wa kudumu lakini uamuzi huo unaonekana kuwekewa chumvi ya kisiasa.
Tanzania/Malawi: Utafutaji Mafuta kwenye Ziwa Nyasa WachocheaMgogoro wa Umiliki
Taarifa kwamba Malawi inatafiti mafuta katika Ziwa Nyasa (linalojulilkana pia kama Ziwa Malawi) zimeibua mjadala motomoto. Wakati ambapo serikali ya Malawi inadai umiliki kamili wa ziwa hilo, Tanzania inataka mpaka utambuliwe kuwa katikati ya ziwa.
Iran: ‘Marufuku Isiyo Rasmi ya Kutembea’ ya Tehran Wakati wa Mkutano wa NAM
Mkutano wa 16 wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote ulianza mnamo tarehe 26 Agosti, 2012 jijini Tehran huku kukiwa na ulinzi mkali. Umoja huo madhubuti (NAM) unaoundwa na nchi ni mabaki ya mvutano uliokuwepo enzi za Vita Baridi kati ya Mashariki na Magharibi, na umoja huu unachukuliwa na Iran pamoja na mataifa mengine kama jukwaa mbadala kwa ajili ya kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali yanaoukabili ulimwengu hivi sasa. Iran inasema inapanga mazungumzo kuhusu mpango wa amani ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, lakini hakuna uwakilishi kutoka upande wa waasi ulioalikwa kwa sababu Tehran ni rafiki wa karibu wa utawala wa Rais Bashar Assad wa Syria.