Obama Barani Afrika: Vita ya Kibiashara na China?

Rais Obama ametembelea bara la Afrika kwa ziara iliyokuwa imepangwa kati ya tarehe 26 mpaka Julai 3, 2013. Hivi karibuni alikuwa nchini Afrika Kusini baada ya kutembelea Senegali na baadae Tanzania. Wachambuzi wengi wanaoiona safari hiyo kama mpango wa kushindana , kama jaribio la Marekani kupambana na mafanikio ya kiuchumi ya China [fr] katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Tangu 2010, China imekuwa mshirika mkuu wa kibiashara barani Afrika [fr], ingawa kwa miaka minne iliyopita, wakati wa ziara ya Obama nchini Ghana, Marekani ilikuwa katika nafasi hiyo. Hotuba ya Obama akiwa Ghana miaka minne iliyopita iliwaacha wa-Afrika na wasiwasi na palikuwa na uwanja mdogo sana unaofanana.

Katika video ifuatayo, mwandishi wa Global Voices Abel Asrat anayeandikia ukurasa wa Global Voices kwa ki-Ahmari alitoa maoni yake kuhusu sera ya Obama kwa bara la AFrika kama ilivyo leo:

Kwenye mtandao wa Twita, wasiwasi wa sababu hasa ya ziara ya Obama barani Afrika ulionekana katika alama ishara ya Wolof  #ObamaTakh yenye maana ya “Kwa sababu ya Obama” na “Shukrani kwa Obama” – iliyoanza kutumika siku kadhaa kabla ya kuwasili kwa Obama mjini Dakar.

Baada ya kuwasili kwake katika ardhi ya Senegali haya yalikuwa maneno yake ya kwanza yaliyotawala mitandao ya kijamii. Kisha hisia zikabadilika, wakati @LebouPrincess, M-Senegali aishiye Washington DC,  aliposisitiza kwenye mtandao wa Twitaon:

Plus impressionnant que l'arrivée du Air Force One c'est le revirement des #kebetu (Twittos en Wolof] lol guemoulene dara [vous êtes versatiles] #ObamaTakh

Kilichokuwa kinasisimusha zaidi kuliko kuwasili kwa dege la Air Force One ilikuwa ni kurejea alama habari #kebtu, (twiti katika lugha ya Wolof) lol guemoulene dara [unatembea sana] #ObamaTakh.

Siku iliyofuata Obama aliweza kwa kiasi fulani kuwasogeza wa-Senegali upande wake kwa kuyataja mapigano ya wa-Senegali wakati wa majadiliano yake na Rais Macky Sall na akisema maneno kadhaa katika lugha ya ki-Wolof: Nio Far (Sisi ni washirika),Teranga (ukarimu) na Jerejef (Asante).

Kiini cha mazungumzo kati ya marais hao kilikuwa ni mgogoro wa Mali, usafirishaji wa madawa ya kulevya na masuala ya kiuchumi  [fr]:

Le président américain Barack Obama a annoncé, jeudi à Dakar, que son administration était en train de « chercher des modalités de reconduction » de l’AGOA [African Growth and Opportunity Act], la Loi américaine sur la croissance et les opportunités en Afrique.
S'exprimant au cours d'une conférence de presse conjointe avec son homologue sénégalais Macky Sall, au lendemain de son arrivée au Sénégal pour une visite officielle de trois jours, le chef de l'Etat américain a indiqué avoir demandé à son administration de travailler pour arriver à une reconduction de l'AGOA.
L'AGOA est un programme unilatéral de préférence commerciale signé par le Congrès des États-Unis et permettant l'exemption de taxes et l'accès à un quota libre pour plus de 6 400 produits provenant des pays éligibles de l'Afrique sub-saharienne.
Le président Obama a par ailleurs réaffirmé la volonté de son administration de travailler à développer les relations commerciales entre son pays et le Sénégal.

Rais wa Marekani, Barack Obama, alitangaza siku ya Alhamisi jijini Dakar kwamba utawala wake kwa sasa “unatafiti mbinu za kujihuisha” katika AGOA (Sheria ya Ukuaji na Fursa Afrika), sheria ya Kimarekani inayotawala masuala ya ukuaji na fursa barani Afrika.
Wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake wa Senegali, Macky Sall, siku moja baada ya kuwasili kwa ziara ya siku tatu nchini humo, Mkuu huyo wa nchi wa Marekani alionyesha kwamba alikuwa ameuomba uongozi wake kuihuisha AGOA. AGOA ni mpango wa pamoja unaojikita katika mipango ya kibiashara inayosainiwa na bunge la Marekani, ukiruhusu msamaha wa kodi na kuruhusu uingizaji wa bidhaa zaidi ya 6,400 kutoka katika nchi mahususi kusini mwa Jangwa la Sahara. Cha zaidi, Rais Obama alieleza kwa mara nyingine shauku ya utawala wake kufanya kazi ya kukuza mahusiano ya kibiashara baina ya nchi yake na Senegali.

Nchini Senegali na kwingineko, sehemu ya mkutano huo wa marais hao na waandishi wa habari iliyozua gumzo, ni pale Barack Obama, kwa uhuru kabisa na kwa namna fulani ya uungwaji mkono na mwenzake wa Senegali, alipogusia masuala ya haki za watu wenye mahusiano ya jinsia moja, mashoga na wasagaji katika bara la Afrika. Sabine Cessou kwenye Rue89 anaeleza namna maswali yalivyochaguliwa [fr] wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari :

Les questions des quelques 300 journalistes présents ne pouvaient pas être posées librement, mais avaient été sélectionnées à l’avance. Ce processus a permis à seulement deux journalistes sénégalais et deux journalistes américains de poser quelques salves de questions chacun.

The questions from the 300 journalists were screened beforehand. The process allowed for two Senegalese journalists and two american ones to ask the tough questions.

Macky Sall’s response did not disappoint Senegalese traditionalists [fr]:

Fondamentalement, c’est une question de société. Il ne saurait y avoir un modèle fixe dans tous les pays. Les cultures sont différentes, tout comme les religions et les traditions.
Même dans les pays où il y a dépénalisation de l’homosexualité, les avis ne sont pas partagés. Le Sénégal est un pays tolérant : on ne dit pas à quelqu’un qu’il n’aura pas de travail parce qu’il est homosexuel. Mais on n’est pas prêt à dépénaliser l’homosexualité. C’est l’option pour le moment, tout en respectant les droits des homosexuels.
Nous ne sommes pas homophobes au Sénégal. La société doit prendre le temps de traiter ces questions sans pression.

Kwa dhati kabisa, hili ni swala la jamii. Isingekuwa rahisi kuwa na mfumo unaofanana kwa kila nchi. Utamaduni ni tofauti, kama zilivyo dini na mila.
Hata katika nchi ambazo zimeuhalalisha ushoga, bado hazifanani kwa mambo kadhaa. Senegali ni nchi ya kuvumiliana: hakuna mtu anaambiwa hatafanya kazi kwa sababu tu ni shoga. Hata hivyo, hatuko tayari kuuhalalisha ushoga. Huo ndio uchaguzi wetu kwa sasa, wakati huo huo tukiheshimu haki zao. Hatuna chuki kwa mashoga nchini Senegali. Jamii lazima ishughulikie masuala haya bila shinikizo.

Nchini Marekani, Kimberly McCarthy alinyongwa jana yake jijini Texas, na maneno yake ya kushutumu hukumu ya kifo yalijenga mfanano: rais wa Senegali alimwambia mwandishi wa habari aliyekuwa akimhoji kwamba nchi kadhaa bado zinakubaliana na hukumu ya kifo -bila kuitaja Marekani – ingawa hukumu hiyo imefutwa nchini Senegali (na mara ya mwisho mtu kuhukumiwa kifo ilikuwa mwaka 1967) na hata hivyo, nchi hiyo imekuwa makini kutohubiri suala hilo kwa wengine.

Wakati @hpenot_lequipe, mwandishi wa jarida la kifaransa l'Equipe, alikuwa na maoni haya kwenye twita:

Très intéressant échange entre Obama et Macky Sall. Pour une fois, un président africain ne s'est pas écrasé devant E-U. Respect.

Mbadilishano mzuri baina ya Obama na Macky Sall. Kwa mara ya kwanza, rais wa Kiafrika asiyetetereka mbele ya Marekani. Heshima kwako.

Na kutoka kwa @Toutankhaton, mwanachama wa waafrika waishio Paris:

Bravo à @macky_sall pour sa réponse cash à @BarackObama ! Peine de mort vs mariage gay! #obamatakh

Heko @macky_sall kwa majibu yake mazuri kwa @BarackObama! Hukumu ya kifo dhidi ya ndoa za jinsia moja! #obamatakh

Ifuatayo ni video ya mkutano na waandishi wa habari iliyowekwa na Xalimasn kutoka Senegali:

http://youtu.be/W_O4ay69OFg

Photos from Obama’s visit can be viewed on the Facebook page of the Dakar Echo.

Nchini Afrika Kusini, mapokezi yake hayakuonekana kuwahamasa kubwa, kama mwanablogu wa mambo ya nje wa jarida la Washington Post Max Fisher anavyoeleza:

Kwa kiasi kikubwa kwenye miaka ya 1980, Marekani na Uingereza zilionekana machoni mwa baadhi ya Waafrika Kusini, kama nchi zilizokaa kimya pasi na sababu, zikivumilia serikali ya ubaguzi wa rangi. Hiyo inaweza kusaidia kueleza kwa nini wakosoaji wengi wa Obama nchini Afrika Kusini wanamkosoa  kwa kuiunga mkono “nchi ya ubaguzi wa rangi” ya Israeli. Makundi kadhaa yanatoa mifano wa mashambulizi ya kivita yanayofanywa na Marekani na mahabusu ya Guantanamo, Cuba.

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.