Habari kuhusu Mahusiano ya Kimataifa kutoka Januari, 2011
Dunia ya Uarabu: “Acheni Kulia Juu Sudani”
Kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudani ya Kusini leo imeiweka nchi hiyo kwenye uangalizi wa karibu miongoni mwa watumiaji wa twita wa Kiarabu. Kuanzia Saudi Arabia mpaka Palestina, watumiaji Twita wa Kiarabu wanajadiliana kuhusu mshikamano, kugawanyika na rasili mali za Sudani.
Sudani: Kura ya Maamuzi ya Uhuru wa Sudani Kusini kwenye Twita
Wapiga kura huko Sudani Kusini walipiga kura ili kuamua ama kujitenga au kubaki kuwa sehemu ya Sudani. Huu ni mkusanyo wa twita zinazohusiana na Kura ya Maoni. Unaweza kufuatilia twita moja kwa moja kwa kutumia alama ya #SudanRef.