Habari kuhusu Mahusiano ya Kimataifa kutoka Julai, 2009
Kameruni: Wanablogu Waijadili Hotuba ya Obama Ghana
Rais wa Marekani Barack Obama alitoa hotuba yake Ghana ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa kama hotuba ya sera yake ya Afrika. Wakameruni wa nyumbani na wale wa ughaibuni wamekuwa wakijadili maneno yaliyotamkwa na Kiongozi wa Marekani mwenye asili ya Afrika kwa kupitia ulimwengu wa blogu.
Afrika: Obama Atumia Nyenzo Mpya za Habari Kuzungumza na Waafrika
“Umeshawahi kutaka kumuuliza kijana wetu wa Nyangoma maswali yoyote? Kwa maneno mengine, je ungependa Rais wa Marekani, Barack Obama ajibu maswali yako?,” ndivyo inavyoanza makala kwenye blogu ya Hot Secrets inayohusu matumizi ya Obama ya zana mpya za habari ili kukutana na kuongea na Waafrika wa kawaida.