Habari kuhusu Mahusiano ya Kimataifa kutoka Juni, 2013
Rais Obama Kuitembelea Tanzania
Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Barack Obama anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam kesho alasiri kwa ziara ya kiserikali. Blogu ya Swahili Time imeweka ratiba ya...
Raia wa Myanmar Wachukizwa na Mashambulizi Dhidi ya Wahamiaji Wenzao Nchini Malasia.
Vurugu za kikabila nchini Mynmar inaonekana kusambaa hata katika nchi za jirani.. Baadhi ya wahamiaji wa Mynmar wa jamii ya budha wanaoishi nchini Malasia wiki chache zilizopita ambapo watu wengi wanaamini kuwa mashambulia hayo yanahusiana mvutano wa kimakabila na kidini unaoendelea nchini Myanmar. Mwitikio wa awali wa serikali ya Myanmar wa kukanusha matukio haya uliwakasirisha watumiaji wengi wa mtandao.
Misri: Wafanyakazi wa Asasi Zisizo za Kiserikali Nchini Misri Wafungwa Jela
Kuhukumiwa kwa wafanyakazi wa ki-Misri na kigeni wanaofanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali (NGO) kifungo cha hadi miaka mitano jela, kumesababisha hasira katika mitandao ya kijamii na katika maeneo mengine. Hatua hiyo imeonekana kama onyo kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na yale yanayokuza demokrasia.
China Yadaiwa Kuchimba Dhahabu Kinyume cha Sheria Nchini Ghana
Shirika la Habari la Xinhua limeripoti kwamba raia 124 wa Kichina waliodaiwa kushiriki katika uchimbaji wa madini haramu ya dhahabu walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Ghana. Serikali ya China imetakiwa kulinda na kuwatetea raia...