Dar es Salaam, ambao ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania, unarejea katika hali yake ya kawaida baada ya siku mbili za kuwa mwenyeji wa mtu anayeaminika kuwa mwenye mvuto mkubwa duniani, Rais wa Marekani, Barack Obama. Mitaa ya jiji la Dar Es Salaam ilihanikizwa na picha za Rais huyu.
Mtumiaji huyu wa Instagramu alinasa picha kwenye miongoni mwa mabango ya barabarani na inaonekana aliridhika sana na mategemeo yaliyopo kuhusiana na ujio wa Obama.
Wakazi wa jiji la Dar Es Salaam walijipanga pembezoni mwa barabara kwa ajili ya kumpokea katika ardhi yao Rais wa kwanza wa Amerika aliye na asili ya Afrika, kama jinsi picha hii iliyowekwa katika ukurasa wa Twita inavyoonesha:
@shurufu: Watanzania wakiwa wamejipanga pembezoni mwa barabara ya Sokoine wakisubiri kumpokea Barack Obama @BarackObama to #Tanzania. #ObamainTanzania #ObamainAfrica pic.twitter.com/yXMtpDE9KO
Obama aliitembelea Tanzania ikiwa ni sehemu ya ziara ya wiki moja kwa mataifa matatu ya Afrika, ambapo ni ziara yake ya kwanza kabisa na kubwa katika bara ambalo ndilo asili yake tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2008. Mapema alipowasili nchini Tanzania Obama alitangaza mpango wa dola za kimarekani bilioni 7 zitakazowekezwa kwenye mkakati wa kuboresha nishati ya umeme katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.. Hili lilitafsiriwa kuwa ni kiini cha uhusiano ambao Marekani ilitaka kuuanzisha na ambao unajengwa kwa uwekezaji na ushirikiano:
@whitehouse: “Mwishowe, lengo kubwa hapa ni kwa Waafrika kuijenga Afrika kwa ajili ya Waafrika.” —Obama in Tanzania: http://at.wh.gov/mz2hT , pic.twitter.com/pnBCU7bSCQ
Wakati wa kuwasili kwake, Obama alikaribishwa vizuri na kwa aina ya kipekee kabisa kama jinsi mwanablogu mpiga picha Issa Michuzi alivyoweza kunasa picha ya hali ilivyokuwa katika uwanja wa kimaifa wa ndege wa Julius Nyerere:
Picha za aina hii zilimfanya mtu mmoja kusema hili :
@bkyeyune: Kwa kuangalia picha mbalimbali mtandaoni, Obama alikuwa na wakati mzuri zaidi Tanzania kuliko alipokuwa Afrika Kusini.
Mvuto wa ujio wa Obama haukuishia tu katika mitaa ya jiji la Dar Es Salaam. Gaure Mdee (@Profesy) alitwiti picha hii kutoka katika mji wa Stone Town, Zanzibar ikionesha watu wakifuatilia ziara ya Obama kupitia Televisheni moja ya Tanzania:
Hata hivyo, si kila mmoja alikubaliana na ujio wa ndugu Obama. Bwana mmoja katika Video ya Youtube ifuatayo iliyopakiwa na Omar A. Mohammed, Karabani, Ras Novatus na John Mahundi, ambao walikuwa wakifanyia shughuli zao karibu na mtaa ambao msafara wa Rais ulipita, alisema kuwa, lengo za ziara ya Obama nchini Tanzania ilikuwa ni kwa msukumo wa malengo yake binafsi na kuwa uwepo wake Tanzania haukuwa na lolote la kuisaidia Tanzania au watu wake.
Mtizamo huu ulionekana kuwekwa na mwanablogu Elsie Eyakuze wa blogu ya The Mikocheni Report ambaye, wiki moja iliyopita aliibua neno ‘ukoloni mamboleo’ katika kuelezea umuhimu wa ziara ya Obama:
Sasa kutakuwa na jukumu kubwa la wafanyabiashara walioambatana na Rais Obama la kutafuta fursa za kibiashara nchini Tanzania. Kuna hali fulani ya kutia mashaka inayotumiwa na Marekani ya kuyahadaa mataifa mengi ulimwenguni…Gesi, Africom, Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Milenia, wafanyabiashara – Hivi ni vitu gani ukizingatia hali tuliyonayo hivi sasa? Ndio, Barack Obama anakuja Tanzania. Kama angeweza kuja na shehena ya kuheshimu haki za raia na kisha kuzidunga moja kwa moja kwenye mishipa ya viongozi wetu, ningeridhika. Lakini, ninafahamu, Rais wa Marekani ana matatizo yake machache ya kuheshimu uhuru wa watu wa Amerika, kwa mfano, upelelezi huru wa Taifa? *dharau.*
Katika Vijana.FM, kulikuwa na manung’uniko kuwa ni kwanini kulikuwa na pilikapilika nyingi katika ujio wa Obama kuliko ilivyowahi kuwa kwa wakuu wanchi wengine waliowahi kuitembelea Tanzania:
Ninaweza kuelewa kuhusu maandalizi ya kina ya kiulinzi kwa ajili yake, lakini ni kweli tunapaswa kufanya usafi eti kwa kuwa kiongozi huyu mashuhuri anaitembelea Tanzania? Ninaelewa kuwa, anakuja kuitembelea nchi yetu na labda ana vitu vizuri kwa ajili yetu, lakini mtizamo wetu kuhusiana na safari yake ni wa kipuuzi kabisa. Ni ujumbe gani tunataka kuyaambia mataifa mengine ya Afrika, na la muhimu sana, kwa ulimwengu? Ni ujumbe gani tunaourithisha kwa watoto wetu, viongozi bado wanajipanga?
Kwingineko, January Makamba, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, akitoa maoni yake katika blogu ya Taifa Letu, alisema kuwa, siyo Tanzania, na pia Afrika yote, inayoihitaji Amerika. Bali ni Marekani ndio iliyoihitaji zaidi Afrika:
Amerika bado inaendelea kuwa Taifa kubwa duniani- angalau kwa wakati huu. Namna mojawapo wa kuendelea kushikilia nafasi hii katika wakati huu ambao dunia si salama na iliyo na ushindani mkubwa wa kiuchumi na kiutamaduni ni kwa kuweka mbele utu. Na hili ndilo tegemeo la Waafika wengi- kwamba Amerika isijenge urafiki na nchi fulani kwa sababu za kiulinzi au kwa ajili ya mikakati fulani tu bali iw ni kwa ajili ya maendeleo yaliyokusudiwa kwa kila mmoja- ya uhuru, usawa, uvumilivu na pamoja na maendeleo ya watu.
Baadhi ya Watanzania walijisikia furaha kwa Obama kuitembelea nchi yao, maoni ya bwana mmoja yaliyomo katika video ifuatayo iliyopakiwa mtandaoni na Omar A. Mohammed, Karabani, Ras Novatus na John Mahundi, aliiongea mara baada ya kuona msafara wa Rais wa Marekani ukipita kuelekea Ikulu:
Jana majira ya jioni wakati Obama alipokuwa anaondoka, Ahmed Salim aliweza (@asalim86) kunasa hisia za watu:
@asalim86: …na Rais wa Marekani ameshaondoka, turudi kwenye taratibu zetu za kawaida hapa #Tanzania
Wakati umuhimu wa ziara yake hapa Tanzania unaendelea kuwa gumzo, inaonekana kama vile Obama ameshajiwekea kumbukumbu ya kudumu katika utambulisho wa Jiji la Dar Es Salaam
@shurufu: #ObamainTanzania: The newly christened Barabara ya Barack Obama. Cc: @BarackObama pic.twitter.com/IuSXycqsL7