Habari kutoka 4 Julai 2013
Raia wa Misri Wamng'oa Morsi Madarakani
Mohamed Morsi, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood siyo tena Rais wa Misri. Morsi ameondoshwa madarakani baada ya kutumikia kwa mwaka mmoja kama Rais mara baada ya maandamano makubwa nchini kote Misri yaliyomtaka kujiuzulu, maandamano hayo yalianza mapema mwezi Juni 30. Mkuu wa majeshi ya Misri, Generali Abdel Fattah Al Sisi, katika matangazo ya mojakwa moja dakika chache zilizo pita, alisema kuwa, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba ndiye atakayekuwa Rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya kitaifa ya Kiteknokrasia itaundwa.
Watanzania Waitafakari Ziara ya Obama Iliyosubiriwa kwa Matumaini Makubwa
Dar es Salaam, ambao ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania, unarejea katika hali yake ya kawaida baada ya siku mbili za kuwa mwenyeji wa mtu anayeaminika kuwa mwenye mvuto mkubwa duniani, Rais wa Marekani, Barack Obama. Mitaa ya jiji la Dar Es Salaam ilihanikizwa na picha za Rais huyu.