Habari kuhusu Palestina

Israel: Kublogu Kwa Ajili Ya Mazingira Nchini Jordan

  16 Disemba 2009

“Wanamazingira na Waandishi kutoka Palestina, Jordan na Israel watakutana huko Madaba, Jordan mwezi huu kwa ajili ya warsha ya siku 2: “Kublogu kwa Ajili ya Mazingira” tarehe 20-21 Desemba,” anaandika Muisrael Green Prophet, kwenye Mideast Youth.

Palestina: Mtaa wa Twita

  15 Novemba 2009

Eman katika AquaCool anatoa maoni kuhusu mtaa wa kwanza kupata jina linalotokana na huduma ya Twita, katika kambi ya wakambizi huko ukingo wa Magharibi.

Palestina: IDF Yachoma Moto Magari Ya Wapalestina

  28 Oktoba 2009

Kwenye Do Unto Others, Samuel Nichols anaandika kuwa doria ya jeshi la Israel imeanza kuchoma moto magari ambayo yanakamatwa yakijaribu kuvuka mpaka kutoka Ukanda wa Magharibikuingia Israel. Ametundika video hapa.

Palestina: Maoni Juu ya Kuzinduliwa Kwa Huduma ya Google.ps

  16 Agosti 2009

Google imeongeza anwani ya google.ps (google palestina) kwenye orodha yake zana inayotoa huduma za utafutaji zinazolenga sehemu mbali mbali. Anwani hiyo mpya inakusudiwa kufanya kazi katika ukanda wea Magharibi na Gaza, ambako watoaji huduma za intaneti hufanyia kazi zao.

Kivu Mpaka Gaza: Namna Vyombo Vya Habari Vinavyochagua Vipaumbele

  11 Januari 2009

Mdahalo unaodadisi ni kwa nini vita katika Mashariki ya Kongo vinapewa kipaumbele kidogo ikilinganishwa na migogoro inayotokea Mashariki ya kati. Mwandishi wa habari wa Rue89 anauliza, "ikiwa kifo cha Muisraeli mmoja ni sawa na vifo kadhaa vya Wapalestina, ni maiti ngapi za watu wa Kongo zitakazowekwa kwenye mnara wa mazishi huko Gaza?" Wanablogu wa pande zote mbili wanalichambua swala hilo.

Serikali Ya Irani Yautumia Mgogoro Wa Gaza Kukandamiza

  11 Januari 2009

Wakati wanablogu kadhaa wa Kiirani (pamoja na wale wa-Kiislamu) waliongeza makala zao na jitihada nyingine za kidijitali, kama vile "Google bomb" kulaani uvamizi wa Israeli katika ukanda wa Gaza, wanablogu wengine wanasema kwamba serikali ya Irani inatumia 'mwanya wa mgogoro wa Gaza' kukandamiza vyombo vya habari na jumuiya za kiraia ndani ya nchi hiyo.

Palestina: Mawasiliano na Gaza

  8 Januari 2009

Katika mazingira ya kawaida bila kiwango kikubwa cha wanaojua kusoma, usambaaji wa intaneti husimama kati ya asilimia 13 mpka asilimia 15 (Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa pamoja). Kutokana na mashambulizi yanayoendelea huko huko Gaza, uwezo wa kutumia intaneti umepungua sana. Japokuwa kuna idadi ndogo ya wanablogu wanaoandika moja kwa moja kutokea Gaza, wakazi wengine wengi wanatumia ujumbe wa maandishi wa simu za mkononi pamoja na simu nje ya nchi katika matumaini kwamba ushahidi wao utapata sehemu ya kuelezwa.

Palestina: Shule ya Umoja wa Mataifa Yashambuliwa na Makombora ya Israeli, Zaidi ya 40 wafariki

  7 Januari 2009

Takriban majira ya saa 12 za jioni (GMT +2), Idhaa ya Kiingereza ya Al Jazeera iliripoti kuwa shule moja ya Umoja wa Mataifa ilipigwa wakati makombora mawili ya vifaru yalipolipuka nje ya shule hiyo. Shule hiyo, iliyopo Jabaliya, ilianza kutumiwa kama makazi ya raia wa Gaza waliozikimbia nyumba zao au waliopoteza makazi yao. Zaidi ya watu 40 wameuawa. Jillian York anawasilisha maoni ya mwanzo kabisa katika ulimwengu wa blogu na twita.