· Juni, 2009

Habari kuhusu Uchaguzi kutoka Juni, 2009

Iran: Video za Maandamano ya Upinzani Zazidi Kumiminika

Zaidi ya watu 100,000 waliandamana mjini Tehran Jumatatu iliyopita ili kumuunga mkono mgombea urais mwanamageuzi, Mir Hussein Mousavi pamoja na madai yake ya kuataka kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi ambayo yalimtangaza rais aliye madarakani Mahmoud Ahmadinejad kama mshindi katika uchaguzi wa tarehe 12 Juni. Damu ilimwagika mwishoni mwa maandamano hayo. Watu wapatao 7 walipoteza maisha yao.

17 Juni 2009

Irani: Maandamano na Ukandamizaji

Mamia ya maelfu ya Wairani mjini Tehran na katika miji mingine kadhaa wameandamana kumuunga mkono mgombea urais Mir Husein Mousavi huku wakiipuuza amri ya serikali inayokataza maandamano. Japokuwa huduma za Twita, FaceBook pamoja na YouTube zimezuiliwa kwa kuzimwa nchini Iran, Wairani wengi wamekuwa wakitumia tovuti-vivuli ili kuvizunguka vichujio vilivyowekwa na wanaripoti habari kadiri zinavyotokea. Utawala wa Irani pia umezuia huduma za jumbe za maandishi kwa kutumia simu za mkononi (SMS), kadhalika utawala huo unachuja tovuti kadhaa zinazoakisi maoni ya wanamageuzi.

16 Juni 2009

Uchaguzi Wa Irani Katika Picha

Uchaguzi wa rais nchini Irani utafanyika tarehe 12 Juni. Ni watu wanne tu kati ya watu zaidi ya 400 waliojiandikisha ambao wamepewa idhini rasmi na Baraza la Walezi kuwa wagombea katika uchaguzi. Macho makali ya wanablogu-wapiga picha yamenasa nyakati na taswira katika mitaa ya Irani ambako watu walikuwa wakiwapigia debe wagombea wanaowapenda.

13 Juni 2009

Msumbiji: Shambulio Dhidi Ya Mgombea Urais

Wanablogu wa Msumbiji wanaandika kuhusu shambulio dhidi ya mwanasiasa Daviz Simango, kwenye mji wa kaskazini wa bandari ya Nacala. Pamoja na maoni kutoka kwenye ulimwengu wa blogu, chama cha Simango pia kilitumia huduma ya Twita kuandika kuhusu shambulio hilo.

13 Juni 2009

Malawi: Wasikilize wanablogu wa uchaguzi Malawi

Wamalawi wanapiga kura katika uchaguzi wa Raisi na Bunge. Baadhi ya wanablogu walipatiwa mafunzo na PenPlus Bytes, Taasisi ya kimataifa ya Uandishi wa TEKNOHAMA kwa ushirikiano na New Media Insitute kwa lengo la kuangalia na kutoa maoni yao kuhusu uchaguzi huo kwa kutumia blogu, teknolojia ya twita na simu za viganjani. Hebu na tuziangalie blogu zao, ambazo zimehifadhiwa katika Potal ya chaguzi za Afrika. Poto hii hutoa taarifa za kutosha kuhusu chaguzi mbalimbali katika nchi za kiafrika.

8 Juni 2009

Uganda: Mke wa Rais ateuliwa kwenye Baraza la Mawaziri

Mabadiliko ya hivi karibuni katika Baraza la Mawaziri limewafanya wanablogu wa Uganda kuanza kubashiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2011. Moja ya uteuzi aliofanya Rais Yoweri Museveni ni ule wa kumteua mke wake, Janet, kuwa Waziri wa Nchi wa Karamoja. Eneo hili liko kaskazini-mashariki mwa Uganda na kwa miongo mingi limegubikwa na migogoro na umaskini uliokithiri.

8 Juni 2009