Habari kuhusu Uchaguzi kutoka Aprili, 2013
Urusi: Wapinzani Wapumbazwa na Uchaguzi wa Awali, Wapoteza Uchaguzi Halisi
Mwezi Agosti (mwaka 2012), Mtandao wa Sauti za Dunia uliripoti habari za wanaharakati kadhaa wanaohusika na vuguvugu la maandamano nchini Urusi wanaogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Walitumaini itakuwa rahisi kushinda uchaguzi huo mdogo, ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Oktoba 14, 2012 huku idadi ya ndogo ya wapiga kura wakiojitokeza tena ndani ya madai ya siku nyingi ya wizi wa kura katika uchaguzi, Warusi walishiriki kwa maelfu katika uchaguzi nchini kote, kupiga kura kuwachagua mameya wa miji, madiwani, na wabunge wa mikoa.
AZISE ya Uwazi Yajiandaa kwa Uchaguzi wa Jumapili Nchini Venezuela
Wakati wapiga kura wa Venezuela wakijiandaa kuelekea kwenye uchaguzi wa mara ya pili katika kipindi cha miezi sita, kikundi cha Asasi Zisizo za Kiserikali kimekusanya nguvu ili kuhakikisha kuwa wanakuza uwazi katika mchakato wa uchaguzi.
Vyama vya Siasa Msumbiji na Matumizi ya Intaneti
(…) kuna nafasi ambayo mpaka sasa haijatumiwa ipasavyo na vyama vya siasa nchini Msumbiji, iwe ni kwa ajili ya kueneza propaganda za kisiasa au kufanya kampeni za uchaguzi: nalo ni...