· Julai, 2012

Habari kuhusu Uchaguzi kutoka Julai, 2012

Wananchi wa Mexico Wanamchagua Rais Mpya

  12 Julai 2012

Mnamo tarehe 1 Julai, Wa-Mexico walipiga kura kumchagua rais wao mpya. Punde tu kura zilipoanza kupigwa, watumiaji wa mtandao wa intaneti walianza kutoa mawazo na uzoefu wao. Walipanga pia namna tovuti na alama ishara za mtandao wa twita zitakavyotumika kukusanya taarifa juu ya udanganyifu na nyendo zilizo kinyume cha sheria wakati wa uchaguzi huo.