Wananchi wa Mexico Wanamchagua Rais Mpya

Mnamo tarehe 1 Julai, Wa-Mexico walipiga kura kumchagua rais wao mpya. Kabla ya kuanza kupiga, hisia za watumiaji wa mtandao zilionyesha kwamba uchaguzi huo utakuwa na ushindani wa karibu kati ya  Enrique Peña Nieto (kwa kifupi, EPN) wa chama cha mageuzi ya kitaasisi na Andrés Manuel López Obrador (kwa kifupi AMLO) wa chama cha mageuzi ya kidemokrasia, ingawa wafuasi wa Josefina Vázquez Mota (kutoka chama kinachotawala sasa) hakupoteza matumaini ya kushinda. Punde tu kura zilipoanza kupigwa, watumiaji wa mtandao wa intaneti walianza kutoa mawazo na uzoefu wao.

Mtumiaji wa twita @YONOFUI alitoa uhakikisho:

Hoy es el primer día de un país q comenzará a madurar y se dará cuenta que sin trabajo ciudadano no habrá logros

Leo ni siku ya kwanza ya nchi ambayo itaanza kukua na kutambua kwamba bila kazi ya wananchi hakutakuwa na mafanikio yoyote.

Alama ishara #Elecciones2012 (uchaguzi 2012) kwa haraka sana ikawa ndio mada iliyotawala mijadala ya mtandao wa twita.

Watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti walianza kuweka utaratibu wa tovuti na alama ishara za mtandao wa twita ili kukusanya habari zinazohusu udanganyifu na namna nyingine za matendo yaliyo kinyume cha sheria kama kufanya kampeni karibu na vituo vya kupigia kura. Tonatiuh Bravo (@tonatiuhbravo)alitumia alama ishara, #Operacion1J, kuripoti hivi:

Quieren documentada la compra de credenciales acá el video #Operacion1J yfrog.us/gh5kgiz

Kama unataka  ushahidi wa ununuzi wa kadi za kupigia, video yake ndio hii#Operacion1J yfrog.us/gh5kgiz

“kura ni bure na siri”. Wamexico  wapiga kura katika kituo cha kupigia kura katika jiji la Mexico mnamo Julai 1, 2012. Picha na Enrique Perez Huerta, hati miliki na Demotix.

Baada ya matokeo ya awali kuanza kutolewa, Vyombo vikuu vya habari kutoka ulimwenguni kote, ikiwa ni pamoja na Mexico, vilikimbilia kutangaza  kwamba Taasisi ya Uchaguzi Nchini humo (IFE) ilikuwa imebashiri kwamba Enrique Peña Nieto atashinda. Wakati wafuasi wake wakisherekea, baadhi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti walikatishwa tamaa na wengine waonyesha tamauki.

Peña Nieto alikimbilia kujitangaza mshindi baada ya asilimia ndogo ya kura kuhesabiwa, akijaza akaunti yake ya twita (@EPN) na matamko ya shukrani na maneno ya ushindi, ambayo yalizua shaka za udanganyifu na wizi wa kura miongoni mwa watumiaji wa mtandao.

¡Muchas gracias a todos los mexicanos! Uds. han hablado y han elegido votar  por un cambio de rumbo.

Shukrani sana kwa Wa-Mexico wote!Mmeongea na kuchagua kupigia kura mabadiliko ya mwelekeo.

Mwanahabari wa kujitengemea Erik de la Regera (@erikdelareguera) aliuliza:

Swali: Tume ya Uchaguzi (IFE) iliwezaje kubashiri ushindi wa Peña wakati ni asilimia isiyozidi 25%  ya kura ndizo zilizohesabiwa na mpambano ukiendelea kuwa mgumu

Wakati mtumiaji ajiitaye Fikiri M-Mmexico (@thinkmexican) ilidokeza hivi:

Kwa kule kumtangaza EPN kuwa ndiye mshindi, AMLO inawekewa shinikizo na vyombo vya habari, Calderón na tume ya uchaguzi kukubali. Haraka yote ya nini? Wanaogopa  nini? Mabadiliko ya kweli?

Matokeo ya mwisho yatatolewa mnamo Jumatano, Julai 4.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.