Habari kuhusu Uchaguzi kutoka Mei, 2013
Je, Baada ya miaka 50, Chama Tawala cha Malaysia Kitashinda Uchaguzi?
Malaysia wnaajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 13 utakaofanyika Mei 5. Maudhui yanayotawala duru za kampeni za uchaguzi huo ni matarajio makubwa waliyonayo wananchi, au 'ubah' kwa lugha ya wenyeji. Je Chama tawala cha Barisan Nasional, kilichokaa madarakani kwa miaka 50, kitaendelea kutawala nchi hiyo?
Uchaguzi Tume ya Uchaguzi Msumbiji: Mwanaharakati Ajitoa Kugombea
Kutokuwepo uwazi na weledi katika mchakato wa kumchagua mgombea, mbali na kufahamika nani hasa watachukua nafasi zinazogombewa kabla hata ya uchaguzi katika taasisi hiyo. Hizo zilikuwa baadhi ya sababu zilizotolewa...
Pakistan: Imran Khan Aanguka na Kuumia Akiwa Kwenye Jukwaa la Kampeni
Aliyekuwa mchezaji maarufu wa kriketi na kisha kuamua kuwa mwanasiasa, ambaye kampeni yake ina tumaini kubwa la kuleta "Pakistan Mpya" aliyeweza kushawishi idadi kubwa ya vijana pamoja na wapiga kura wanaotokea mijini katika mikutano yake, alivunjika vifupa vitatu vya uti wa mgongo pamoja na mbavu baada ya kuanguka kutoka kwenye winchi iliyokuwa katika kimo cha futi 15 mda mfupi kabla ya kuhutubia. tukio hili limeonekana kuliunganisha tena taifa hili lililojigawa kwa visasi vinavyotokana na uchaguzi utakaofanyika mapema wiki hii.
Wagombea wa Urais katika Uchaguzi wa Madagaska
Habari Mpya: Hapa ni orodha kamili ya wagombea 49 [fr] wanaowania nafasi ya Urais katika uchauzi ujao. Orodha hiyo haina jina la rais wa sasa wa mpito. Siku ya mwisho ya...