Habari kuhusu Uchaguzi kutoka Machi, 2010
Martinique: Uchaguzi, utata na kugomea uchaguzi
Jumapili ya tarehe 14 Machi, raia wote wa Ufaransa wakiwemo wale wa idara za ng’ambo za Ufaransa walitakiwa kupiga kura... Lakini michakato miwili ya uchaguzi katika kipindi cha miezi mitatu inaweza kuwachosha 55.55% ya wapiga kura wa Martinique ambo waliamua kubaki majumbani.
Mwaka Mmoja Baada ya Mapinduzi, Viongozi wa Madagaska Wakabiliwa na Vikwazo
Machi 17, 2009 nchini Madagaska, vikwazo vinavyowalenga viongozi wa sasa wa Madagaska vinaandaliwa kwa kushindwa kwao kuheshima makubaliano ya Maputo ambayo hapo awali yalifikiwa na pande zote zinazohusika. Matokeo ya vikwazo hivyo ni pamoja na kuzuiwa kwa mali zinazozalisha fedha na pengine kukamatwa kwa wanaohusika endapo watasafiri nje ya nchi.
Sudani: Je, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Itafanya Kazi?
Jarida la The Financial Times liliripoti hivi karibuni kuwa mpango wa mamilioni ya dola wa Benki ya Dunia wa kusambaza kompyuta na upatikanaji wa Intaneti huko Juba, mji mkuu wa Sudani ya Kusini, umeshindwa. habari hizi zinazua swali: kelele zinazoambatana na teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) zina uhalali?
Iraki: Ni Siku ya Uchaguzi Kwenye Twita
Ni siku ya uchaguzi nchini Iraki na ulimwengu wa Twita umekuwa uking’ong’a na habari mpya mpya tangu mapema asubuhi. Waandishi wa habari na wanahabari wa kijamii walijaribu kutumia Twita ili kutupasha habari kuhusu mambo yanavyotukia nchini humo.