Iran: Video za Maandamano ya Upinzani Zazidi Kumiminika

Zaidi ya watu 100,000 waliandamana mjini Tehran Jumatatu iliyopita ili kumuunga mkono mgombea urais mwanamageuzi, Mir Hussein Mousavi pamoja na madai yake ya kuataka kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi ambayo yalimtangaza rais aliye madarakani Mahmoud Ahmadinejad kama mshindi katika uchaguzi wa tarehe 12 Juni. Damu ilimwagika mwishoni mwa maandamano hayo. Watu wapatao 7 walipoteza maisha yao.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka idhaa ya televisheni ya Uingereza Channel 4 (iliyotangazwa bila kujali amri ya kuyazuia mashirika ya nje kutangaza habari) umati wa watu ulitupa mawe na kuchoma moto jingo linalomilikiwa na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali, wajulikanao kama Basij. Mwanamgambo aliyevalia kofia ya chuma aliyekuwa kwenye paa ya nyumba alipiga risasi hewani kabla ya kujificha ili kuepuka mvua ya mawe. Katika YouTube kuna video nyingi zinazoonyesha jinsi shambulio hilo lilivyotokea:

Asubuhi baada ya tukio hilo la kutupiana risasi, wafanyakazi wa hospitali ya Rasool Akram mjini Tehran waliandamana kupinga mauaji yaliyotokea. Muandamanaji mmoja alibeba bango linalosema “mashahidi 8”

Kupigwa risasi au kukandamizwa hakujazuia mwamko wa upinzani, na maelfu waliandamana tena mjini Tehran siku ya Jumanne. Maandamano ya upinzani yanaongezeka katika miji mingine pia. Katika mji wa Shiraz, wapinzani wanaoonyeshwa katika video hii waliichoma moto picha ya Ahmadinejad.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.