Irani: Kimbunga cha Maandamano Baada Ya Uchaguzi


Maelfu ya watu waliandamana mjini Tehran, Mashdad na kwenye miji mingine mikubwa ya Irani ili kupinga ushindi wa Rais Mahmoud Ahmadinejad katika uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa. Washindani wawili wanamageuzi pamoja na mashabiki wao wanasisitiza kwamba palitokea udanganyifu.

Mir Hussein Mousavi, mpinzani mkuu wa Ahmedinejad alisema kuwa matokeo yaliyotolewa na “waangalizi wasioaminika” yanaakisi “udhaifu wa nguzo zinazosimamisha mfumo mtakatifu” wa Irani na “utawala wa mabavu.” Matukio kadhaa ya kupigana mitaani na maandamano yamewekwa kwenye YouTube.

Maandamano katika mtaa wa Valiasr mjini Tehran ambako maelfu ya waandamanaji walipinga kwa kuimba kauli mbiu dhidi ya serikali ya Ahmadinejad.

Na hapa watu waliimba: ‘Mousavi, rejesha kura yangu!’.

Vyombo vya usalama vilidhibiti waandamanaji:

Maandamano mengine yalifanyika mjini Mashad ambako waandamanaji waliwaomba wanausalama wawaunge mkono [badala ya kuwadhibiti].

Ghomar Ashegahne amechapisha picha kadhaa zinazoonyesha wanausalama wakiwapiga waandamanaji (tazama picha hapo juu). Mwanablogu huyo anaandika [fa] kwamba udhibiti ungekuwa ni sababu nzuri ya kutokwenda kwenye maandamano, lakini ‘tufanye nini na uchungu huu?’

Anasema kuwa Karoubi na Mousavi [wanamageuzi wawili waliogombea] walitaka kubadili hali nchini, na inawabidi waanze sasa.

Belgiran anaandika [fa] kwamba Kiongozi wa Irani, Ali Khamenei, alimpindua Mousavi hata kabla hajakuwa rais na akamweka Ahmadinejad… Anaandika, “Utawala huu umepoteza uaminifu mdogo uliokuwepo.”

Mehrdadd anaandika kwenye Twita, kwamba kiongozi wa Irani anaonyesha kuwa yuko dhidi ya watu wa Irani. Na sasa kila mwanasiasa anapaswa achukue msimamo ulio kwa ajili ya wananchi au dhidi ya wananchi.

Mehri912 anasema kwenye Twita, “Kama Irani italala usiku wa leo, basi ndiyo italala daima”.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.