Irani: Maandamano na Ukandamizaji

Tehran protests, via jomhour.info

Tehran protests, via jomhour.info


Mamia ya maelfu ya Wairani mjini Tehran na katika miji mingine kadhaa wameandamana kumuunga mkono mgombea urais Mir Hussein Mousavi huku wakiikupuuza amri ya serikali inayokataza maandamano. Waandamanaji wanadai kubatilishwa matokeo ya uchaguzi wa rais, wakisema kuwa ushindi wa Rais Mahmoud Ahmedinejad katika uchaguzi wa tarehe 12 Juni ulipatikana katika njia sizizo halali. Majeshi ya usalama yamewashukia wanaandamanaji, na mtu mmoja aliuwawa mjini Tehran leo.

Japokuwa huduma za Twita, FaceBook pamoja na YouTube zimezuiliwa kwa kuzimwa nchini Iran, Wairani wengi wamekuwa wakitumia tovuti-vivuli ili kuvizunguka vichujio vilivyowekwa na wanaripoti habari kadiri zinavyotokea. Utawala wa Irani pia umezuia huduma za jumbe za maandishi kwa kutumia simu za mkononi (SMS), kadhalika utawala huo unachuja tovuti kadhaa zinazoakisi maoni ya wanamageuzi.

Iran09 aliandika katika ujumbe wa Twita mapema leo:

“Nimethibitisha kwamba kuna Basij [wanamgamo wa Kiislamu] waliopo kwenye viwanja na wanawapiga watu kutokea kwenye mapaa ya nyuma. #iranelection”

Jadi aliandika ujumbe wa Twita:

“Watu bado wanajiunga na maandamano. Wanaimba ‘Mousavi! Mousavi! Ichukue kura yangu’ #iranelection”

Mousavi aliongea na kuomba matokeo ya uchaguzi yaangaliwe tena. Alisema yuko tayari kushiriki katika uchaguzi mpya. Kuna filamu za video zinazohuzu uchaguzi hapa.

Kadri upinzani unavyozidi ndivyo ukandamizaji unavyoongezeka
Wanafunzi waliopinga uchaguzi wa rais katika vyuo vikuu mbalimbali walishambuliwa na vikosi vya usalama. Ifuatayo ni video inayoonyesha bweni la Chuo Kikuu cha Tehran jumapili usiku.

Habari mpya: Huu ni mlolongo wa picha kwenye huduma ya Flickr unaoonyesha uharibifu uliofanywa na vikosi vya usalama katika mabweni ya Chuo Kikuu cha Tehran jumapili usiku. Kwa mujibu wa mtumiaji wa Flickr, Agha Hadi, wanafunzi wengi walitiwa mbaroni.

Ifuatayo ni filamu inayoonyesha mwanamke wa Ki-Irani anavyopambana na vikosi vya usalama kwenye kituo cha basi.

Azarmehr anatoa maoni juu ya filamu hii:

Muangalie huyu simba-jike jasiri wa Ki-Irani, kwanza anapiga teke halafu anampiga teke la pembeni askari mtuliza ghasia anayefanana na mtu wa kale aliyebeba rungu! Anapigwa marungu machache lakini hiyo ndiyo thamani ya uhuru an hajali. Na ibarikiwe nchi yetu ya Irani, kwa kuwa na mabinti kama hawa. Woga umetoweka na kasi inapamba moto.

Shukrani kwa Tehranlive kwani tumepata picha kadhaa za Wairani wanaopinga na za mwamko wa upinzani:

Green Vote alituma ujumbe wa Twita [fa] kwamba moja ya kauli mbiu ni, ‘Usiogope, tupo pamoja’. Green Vote pia alituma ujumbe mwingine wa Twita unaosema kwamba Mohammad Ali Tarekh, mwanafunzi mwanaharakati, alitiwa mbaroni kwenye jimbo la Shiraz.

Wanablogu kadhaa kama vile Zeitoon, waliripoti [fa] kwamba watu waliimba Allah-O-Akbar (Mungu Mkubwa) kutokea majumbani mwao nyakati za usiku. Mousavi aliwataka watu waimbe Allah-O-Akbar kutokea kwenye mapaa ya nyumba zao. Wkati wa mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1978-79 watu walikuwa wakifanya hivyo kama ishara ya upinzani dhidi ya Shah.

Obama yuko wapi?
Mwanablogu wa Kimarekani, View from Iran anaandika:

Ninafahamu kwamba maneno matamu ni maneno matamu tu. Kwamba maneno ya rais huwa hayabadili historia japokuwa huwa ni sehemu [ya historia]. Kama kungelikuwa na wakati muwafaka kwa Obama kuwasha uwezo wa maneno yake matamu ni sasa. Leo saa 10 jioni kulikuwa na maandamano katika miji 20 ya Irani. Rafiki zangu *wanataka kuwepo mabarabarani.* Ni wazazi, wafanyakazi wa serikali, wahasibu, wapokezi, naam na wanafunzi pia. Mwisho wake, ukizingatia ghasia zote hizi, sina hakika kwamba wataendelea kujitokeza.
Kwa hiyo Obama, washa uwezo wako wa kuhamasisha. Tumia uwezo wako wa maneno matamu kuwaambia Wairani kuwa, japokuwa hatutatuma majeshi, nyoyo zetu zi pamoja nanyi. Najua kuwa unaweza kufanya kazi vizuri zaidi yangu.


Mateso ya Isfahan

Tehran siyo mji pekee ambako watu wanaopinga wanakandamizwa. Waandamanaji mjini Isfahan, pia wanalengwa na vikosi vya usalama.

Iranevents imechapicha picha kadhaa za maandamano huko Irani. Watu wanafukuzwa na vikosi vya usalama.

na hii pia:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.