Habari kuhusu Kiingereza kutoka Novemba, 2013
PICHA: Mkutano wa Chama Kikuu cha Upinzani Msumbiji cha Shambuliwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia
Mkutano wa hadhara wa mwisho kwa kampeni ya umeya wa chama cha upinzani cha MDM katika Beira ulimalizika kwa watu watatu kuuawa na kadhaa kujeruhiwa – waliojeruhiwa ni pamoja na mwana wa mgombea – kufuatia mashambulizi ya polisi wa kutuliza ghasia ambao walitumia mabomu ya kutoa machozi na kufyatua risasi...
Tajikistan: Wapiga Kura Wana Haki ya Kujua Kama Wagombea “Wameshiba’ au ‘Wana Njaa’
Kama mtandao wa Sauti za Dunia ulivyoripoti, baadhi ya raia wa mtandaoni wanasema watampigia rais anayemaliza muda wake wakati wa uchaguzi wa Novemba 6 katika Tajikistan kwa sababu “kiongozi aliyeshiba ni bora kuliko aliye njaa”. Kutafakari juu ya hili, Salimi Aioubzod anadokeza [tj] ni “huzuni” kuwa wapiga kura katika nchi...
Waathirika wa Kimbunga Nchini Ufilipino Wauliza: ‘Iko Wapi Serikali Yetu?’
Misaada inamiminika kutoka duniani kote lakini bado wahanga wa kimbunga wanalalamika kuwa hawajapokea msaada wowote kutoka serikalini
India: Watu Zaidi ya Milioni 60 Wanaugua Ugojwa wa Kisukari
Ikiwa na watu zaidi ya milioni 60 wanaougua ugojwa wa kisukari [pdf] na wengine wanaokadiriwa kufikia milioni 77 walio katika hatihati ya kuugua ugojwa huu, nchi ya India inajikuta katika vita kali ya kukabiliana na janga la ugonjwa wa kisukari. Katika siku ya ugonjwa wa Kisukari Duniani inayoadhimishwa kila tarehe...
Udadisi wa Sami Anan
Mwanablogu wa Misri Zeinobia anatoa maoni yake machache kuhusu kuibuka tena kwa Sami Anan, Mnadhimu mkuu wa zamani wa Majeshi ya Misri. Je, ana mpango wa kugombea urais? Mwanahabari wa Sauti za Dunia Mtandaoni Victor Salama anasimulia zaidi.
Global Voices Yasaidia Wahanga wa Haiyan Nchini Ufilipino
Kimbunga kijulikanacho kama Haiyan hadi sasa kimeshaua maelfu ya watu nchini Ufilipino. Wiki hii tunaongea na waandishi wetu wlioko nchini Ufilipino pamoja na mfanyakazi anayehusika na misaada kujua ni kwa namna gani tunaweza kutoa msaada wetu.
Misri: “Morsi Hatarudi Madarakani”
Aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi hatarudi madarakani, anasema mwanablogu wa Misri Alya Gadi, kwenye mtandao wa Twita. Kuufanya ujumbe wake wazi, ametafsiri kwa lugha mbalimbali: مرسي لن يعود – Morsi is not coming back – Morsi no va a volver – Morsi ne reviendra pas – Morsi kommt nicht zurück...
FIFA Yazipiga Faini Croatia na Ugiriki kwa Tabia ya Mashabiki ya Ubaguzi wa Rangi
Mnamo Novemba 2013, Croatia ilijiunga na orodha ya kuongezeka kwa timu za taifa za kandanda ambazo FIFA imezipiga faini kwa ajili ya tabia za ubaguzi wa rangi ya mashabiki wao au wajumbe wa timu. Mwezi Mei 2013, FIFA ilianza kutekeleza vikwazo vikali dhidi ya ukabila na ubaguzi. Rais wa FIFA...
Serbia Yaibua Maswali Ikiwa Kanisa Lastahili Kusamehewa Kodi
Nchini Serbia ripoti ya uchuguzi uliofanywa na shirika la Serbia la kila siku liitwalo Blic ikiwa Kanisa la Kisabia la Orthodox, ambao viongozi wao hivi karibuni wamekuwa katika vyombo vya habari mara nyingi kutokana na ripoti ya matumizi ya anasa yaonyesha sasa lazima kuanza kulipa kodi. Kanisa la Kisabia la...
Huzuni na Hasira Mjini Kidal, Mali
Mwanablogu Wirriyamu anaomboleza kuuawa kwa waandishi wa habari wawili wa ufaransa [fr] mjini Kidal, Mali. Lakini kando na huzuni yake kubwa, Wirriyamu pia anajisikia hasira kwa kuona kaskazini mwa Mali inaendelea kutaabika tena kwa mashambulizi ya kigaidi. Anaandika kuhusu hasira ya kimya chake kuhusu hali ya mambo: Tant qu’il ne...