Serbia Yaibua Maswali Ikiwa Kanisa Lastahili Kusamehewa Kodi

Nchini Serbia ripoti ya uchuguzi uliofanywa na shirika la Serbia la kila siku liitwalo Blic ikiwa Kanisa la Kisabia la Orthodox, ambao viongozi wao hivi karibuni wamekuwa katika vyombo vya habari mara nyingi kutokana na ripoti ya matumizi ya anasa yaonyesha sasa lazima kuanza kulipa kodi. Kanisa la Kisabia la Orthodox taasisi zingine zote za kidini yana msamaha wa kutolipa kodi nchini Serbia na mamlaka ya serikali ya kodi hawajawahi kukagua fedha ya jamii yoyote iliyosajiliwa kidini nchini humo. Faida hizi, hata hivyo, hutumika tu kwa bidhaa na huduma zinazotumika kwa ajili ya shughuli za kidini, wakati Kanisa la Serbia la Orthodox inajulikana kuwa na aina mbalimbali za magari ya gharama kubwa katika umiliki wa Kanisa, zinazotumiwa na viongozi wake na wafanyakazi. Katika uchaguzi wa umma uliofanywa na Blic mapema mwezi Novemba 2013, 83% ya washiriki walisema Kanisa la Kisabia la Orthodox wanapaswa kulipa kodi.

Takribani makadirio, inayotokana na kauli ya vigogo wa kanisa, inaonyesha kuwa tu kutoka kwa VAT kwenye mauzo ya vitabu na bidhaa nyingine katika maduka ya kanisa, kama vile faida ya kodi, bajeti ya Jamhuri inaweza kuwa tajiri kwa dinar zipatazo bilioni 10 (€ 6,400,000 / dola milioni 8.5).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.