India: Watu Zaidi ya Milioni 60 Wanaugua Ugojwa wa Kisukari

Ikiwa na watu zaidi ya milioni 60 wanaougua ugojwa wa kisukari [pdf] na wengine wanaokadiriwa kufikia milioni 77 walio katika hatihati ya kuugua ugojwa huu, nchi ya India inajikuta katika vita kali ya kukabiliana na janga la ugonjwa wa kisukari. Katika siku ya ugonjwa wa Kisukari Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 14 Novemba, India imedhamiria kukabiliana na janga la kuongezeka kwa wagonjwa wa kisukari ambao kwa sasa ni tishio nchini humo.

Mwandishi na mwanablogu Prem Rao, aweka bayana dalili anuai za ugonjwa wa kisukari na apendekeza kuwa, kwa wale wote ambao hawajapima kiwango cha sukari/ ugonjwa wa kisukari katika kipindi cha miezi sita iliyopita, bila kupoteza muda, wakapime.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.