Tajikistan: Wapiga Kura Wana Haki ya Kujua Kama Wagombea “Wameshiba’ au ‘Wana Njaa’

Kama mtandao wa Sauti za Dunia ulivyoripoti, baadhi ya raia wa mtandaoni wanasema watampigia rais anayemaliza muda wake wakati wa uchaguzi wa Novemba 6 katika Tajikistan kwa sababu “kiongozi aliyeshiba ni bora kuliko aliye njaa”. Kutafakari juu ya hili, Salimi Aioubzod anadokeza [tj] ni “huzuni” kuwa wapiga kura katika nchi wasiwasi wao zaidi ni kuhusu “shibe” au “njaa” ya mgombea urais= kuliko kuhusu jukwaa la mgombea. Hata hivyo mwanablogu anasema kuwa kama wapiga kura wanataka kujua namna mgombea wao “alivyoshiba” basi wana haki ya kujua hayo:

…itakuwa vizuri kama Tume ya Mpito ya Uchaguzi na kura ya maoni ya Tajikistan (CCERT) kuwataka wagombea wote wa urais kutangaza mapato yao ya kila mwaka na vyanzo vyake …

Kutangaza kwa umma mapato ya mgombea na asili yake, mali yao halisi, na akaunti ya benki yao itaruhusu [wapiga kura], ili kuona kama mgombea ni “kashiba” au “njaa” tupu…

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.