Waathirika wa Kimbunga Nchini Ufilipino Wauliza: ‘Iko Wapi Serikali Yetu?’

Resident of eastern Samar have set up temporary shelters after the storm. Image from Plan Philippines

Wakazi wa mashariki Samar wameanzisha makazi ya muda mfupi baada ya dhoruba. Picha kutoka kwa Mpango wa Ufilipino

Siku sita zimepita tangu kimbunga kikubwa kijulikanacho kwa jina la Haiyan (Yolanda) kuikumba sehemu ya kati ya Ufilipino lakini misaada ya kibinadamu bado haijafika kwa waathirika wengi. Miili mingi ya maiti bado imelazwa katika mitaa, wakimbizi wakiomba chakula, juhudi za kuokoa hazifikii visiwa vingine mbali ya mikoa ya Visayas.

Haiyan ilisababisha dhoruba kama tsunami kuongezeka ambayo iliwauwa maelfu papo hapo. Mikoa ya Leyte na Samar ni miongoni mwa maeneo mengi iliyoathirika vibaya na vijiji vingi kuharibika na kubaki nyika. Kwa mujibu wa ripoti rasmi za hivi karibuni, zaidi ya watu 2,000 wamefariki lakini majeruhi wanaweza kuwa zaidi kwa sababu maiti mingi bado haijapatikana.

Kuna hali ya sintofahamu inayosababishwa majibu yaliyochelewa kutoka serikali lakini baadae yakajitokeza kwenye vyombo vya habari vya kijamii:

Misaada inamiminika kutoka duniani kote lakini hakuna mfumo madhubuti wa usambazaji wa rasilimali hizi:

Vijimambo kwamba hakuna hatua inayoonekana kwa unafuu. Hakuna jitihada kubwa au utaratibu kwa ajili ya misaada. Ni hali ya kushangaza’- @sanjuncssr #YolandaPH
— Tudla Productions (@tudlaprod) Novemba 13, 2013

Wakati Tacloban ikiwa haina maafa, visiwa vingine vimeharibiwa pia na hali ya huko haijaripotiwa vya kutosha. Ayi Hernandez alitembelea jimbo la Capiz na anatoa uchunguzi wake:

Nyumba zilizotengenezwa kwa vifaa vyepesi zilikuwa bapa kwenye ardhi au kuharibiwa sana. Nyumba zilitengenezwa kwa saruji zilinusurika nguvu lakini zilipoteza sehemu ya paa zao kwa au kabisa. Uharibifu ulikuwa wa kusikitisha kidogo wakati tunaingia manispaa ya Ivisan.

Baadhi ya familia zilikuwa zikijenga mahema katika barabara kuu na labda kwa sababu zaidi ya nyumba zilizokuwa zimejengwa kwa vifaa vyepesi, mandhari ilikuwa ya kufadhaisha.

Kwa aina hii ya uharibifu, kilicho tushangaza ni kuonekana kwa kukosekana kwa operesheni ya msaada katika manispaa hizo. Hakuna msaada uliopatikana.

Chini ni baadhi ya picha katika Samar, jimbo ambalo lilikuwa la kwanza kukumbwa na kimbunga Haiyan:

Wafilipino wanashukuru kwa msaada uliotolewa na nchi nyingi.

Image from Facebook of Jeffrey Cruz

Picha kutoka mtandao wa Facebook wa Jeffrey Cruz

Ruffy Biazon, afisa wa serikali, anaandika anachofikiri chafaa kifanyike hivi karibuni:

Wakati shughuli za kutoa misaada zinaendelea na kila mtu ameingilia katika kutoa mkono wa msaada, mi muhimu pawepo na mtu amekaa nyuma, kuangalia nini kilichotokea na utafiti wa nini kilichokwenda mrama, kile kisichokwenda ipasavyo na nini cha kufanya ili kuzuia cha kuzuilika, kujiandaa kwa matukio yanayoweza kuepukika na kutoa rasilimali kwa yanayoweza kufanyika.
Hii lazima kufanyika katika ngazi ya kitaifa na muhimu zaidi, katika ngazi za mitaa

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.