Mnamo Novemba 2013, Croatia ilijiunga na orodha ya kuongezeka kwa timu za taifa za kandanda ambazo FIFA imezipiga faini kwa ajili ya tabia za ubaguzi wa rangi ya mashabiki wao au wajumbe wa timu. Mwezi Mei 2013, FIFA ilianza kutekeleza vikwazo vikali dhidi ya ukabila na ubaguzi. Rais wa FIFA Sepp Blatter alisema hivi karibuni kwamba chama cha kimataifa zinazosimamia asasi lazima zitoe adhabu kali kupambana na masuala haya, na kuongeza kuwa FIFA kwa sasa iko tayari “kuondoa timu kutoka ushindani au kupunguza pointi” kufuatia athari hiyo. Al Jazeera inaripoti maelezo zaidi kuhusu faini iliyotolewa kwa vyama kitaifa vya soka vya Croatia na Ugiriki:
FIFA ililipiga faini Shirikisho la Soka la Croatia 35,000 faranga ya Uswisi ($ 38,000) kwa ajili ya matukio wakati wa kushindwa kwake kwa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji nchini Zagreb Oktoba 11.
“Wafuasi wa Kikroeshia walionyesha saluti ambazo zilitumika wakati wa Vita Kuu vya II na harakati mabavu ya Ustase,” kundi la mashabiki la ufuatiliaji liliripoti kwa FIFA.
FIFA iliipiga faini shirikisho la Kigiriki 30,000 faranga ya Uswisi ($ 32,500) kufuatia taarifa ya mabango yaliyoonyeshwa wakati Ugiriki iliwashinda Slovakia 1-0 mjini Athens Oktoba 11.