Mosi Simba

makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba

Saudi Arabia: Mfalme Awaahidi Wananchi wa Saudia Fedha Zaidi

Fedha zaidi zimeahidiwa kutolewa kwa wananchi wa Saudia, ahadi ambayo Mfalme Abdulla ameitoa kupitia hotuba yake kwa taifa leo. Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi, Mlinzi wa Misikiti Miwili Mitukufu aliwashukuru viongozi wa dini, waandishi na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa juhudi walizofanya kutetea ufalme. Matamko na Amri vilifuata ya kwamba mabilioni yatagawanywa kwa watu wa Saudia.

Urusi: Wanablogu wakutana na Balozi wa Irani, waepa kuhoji masuala nyeti

Mkutano kati ya wanablogu wanaoongoza nchini Urusi na Balozi wa Irani jijini Moscow, siku tatu tu baada ya mwanablogu Hossein Derakshan kuhukumiwa kifungo cha miaka 19.5 jela kwa kile kilichoelezwa kuwa ni "kufanya propaganda zinazoipinga serikali" ulizionyesha wazi juhudi zisizoeleweka za diplomasia ya mtandaoni ya Irani nchini Urusi. Vilevile ulionyesha jinsi maslahi binafsi ya kibiashara pamoja na mtizamo taharuki uliopita kiasi wa baadhi ya wanablogu maarufu wa Urusi.

Tanzania: Matumizi ya Vyombo vya Habari vya Kijamii kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010 Nchini Tanzania

Tanzania inaelekea katika uchaguzi wake mkuu mnamo Oktoba 31 mwaka huu na hivi sasa kampeni za uchaguzi zinaelekea kileleni. Wakati kampeni zikipamba moto, wagombea wa nafasi ya urais, ubunge na udiwani wameanza kutumia zana mpya za mawasiliano ya jamii ili kuwasiliana na wapiga kura. Sanjari na mikutano ya kampeni, ambayo hulenga watu wengi zaidi, idadi ndogo ya wanasiasa wameanza kutumia zana za mawasiliano ya kijamii kama vile blogu, picha za video za mtandaoni, Facebook na Twitter ili kukuza mawasiliano na wapiga kura.

Irani: Huenda Mwanablogu Aliyefungwa, Hossein Derakhshan (”Hoder”), Akakabiliwa na Hukumu ya Kifo

Mwendesha mashtaka huko Tehrani anataka mwanablogu wa Irani aliye gerezani Hossein Derakhshan ("Hoder") apewe adhabu ya kifo. Hakimu bado hajatoa uamuzi. Derakhshan anashtakiwa kwa kosa la “kushirikiana na dola adui, kutangeneza propaganda dhidi ya utawala wa Kiislamu, kutusi utukufu wa dini, na kutengeneza propaganda kwa ajili ya matumizi ya vikundi vinavyopinga mapinduzi." Alitiwa nguvuni miezi 22 iliyopita.

Tunisia: Picha ‘Zilizochakachuliwa’ ni Dalili ya Hali Halisi katika Vyombo vya Habari vya Kitaifa

Utumiaji vyombo vya habari vya kitaifa nchini Tunisia kama chombo vya kupigia propaganda ni jambo ambalo limeripotiwa vya kutosha. Ushahidi wa hivi karibuni kabisa wa utumiaji mbaya wa vyombo vya habari umewekwa bayana na wanablogu wa nchi hiyo mnamo tarehe 20 Agosti baada ya magazeti ya Le Temps na Assabah kuchapisha ripoti kuhusu taasisi ya hisani ya Zeitouna kutuma msaada wa kibinadamu wa chakula kwa waathirika wa mafuriko nchini Pakistani.