Ni mpenzi wa lugha ya Kiswahili. Licha ya kuwa ni mhariri na mwandishi wa vitabu, mimi pia ni mfasiri. Nafasiri maandiko kutoka lugha ya Kiingereza kuja Kiswahili na kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Pia ni mwanablogu: http://simbadeo.wordpress.com Ndiyo kusema kuwa ninapenda kuperuzi kwenye kurasa za mtandaoni ili kuilisha akili kwa habari mbalimbali zinazojiri huku na huko duniani. Ni raia wa Tanzania na mkaazi wa Dar es Salaam. Karibu.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Juni, 2009
Uganda: Mke wa Rais ateuliwa kwenye Baraza la Mawaziri
Mabadiliko ya hivi karibuni katika Baraza la Mawaziri limewafanya wanablogu wa Uganda kuanza kubashiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2011. Moja ya uteuzi aliofanya Rais Yoweri Museveni ni ule wa kumteua mke wake, Janet, kuwa Waziri wa Nchi wa Karamoja. Eneo hili liko kaskazini-mashariki mwa Uganda na kwa miongo mingi limegubikwa na migogoro na umaskini uliokithiri.